Haki za binadamu

Wahamiaji wa Usomali Kenya kufadhiliwa na UNHCR msaada wa $20 milioni

Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) kwenye ziara yake rasmi nchini Kenya wiki hii alitangaza kwamba watafadhilia msaada wa dola milioni 20 kutumiwa kukidhi mahitaji ya wahamiaji wa Usomali pamoja na jamii ya wenyeji wao waliopo Kenya

Kamishna wa Haki za Binadamu aingiwa wahka na ripoti za fujo Nigeria

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay, ametangaza hii leo kutoka Geneva ya kwamba ana wahka mkubwa kuhusu ripoti alizopokea, juu ya taathira za kufumka kwa vurugu ikichanganyika na hali mbaya ya raia iliotanda majuzi katika eneo la Nigeria kaskazini, kufuatia mashambulio ya wafuasi wa kundi la kidini linaloitwa ‘Boko Haram\'.

Hatua za dharura zahitajika kupunguza shida za ajira kwa wafanyakazi wahamaji waliopo nje, inasihi UNCTAD

Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo, (UNCTAD) limearifu kwamba muongezeko wa ukosefu wa kazi ulimwenguni kwa sababu ya kuzorota kwa shughuli za kiuchumi katika soko la kimataifa, ni hali inayosababisha fungu kubwa la wafanyakazi waliohamia nchi za nje kuamua kurudi makwao.

Watoto waliopo vizuizini Rwanda kusaidiwa mawakili na mradi wa UM

Kadhalika Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeripoti kwamba linaunga mkono, na kuahidi pia kuusaidia ule mradi ulioanzishwa na Wizara ya Utawala wa Sheria ya Rwanda, wa kuwapatia watoto 600 ziada waliomo vizuizini, mawakili wa kuwatetea kesi zao.

UM kuisaidia Angola kuhudumia raia maji safi

Mradi wa Pamoja wa Mashirika ya UM Kuhudumia Maji na Usafi umeanzishwa rasmi karibuni nchini Angola.

Msomi wa Kenya, Ngugi wa Thiong'o, ajumuisha maoni binafsi juu ya 'wajibu wa kimataifa kulinda pamoja raia'

Alkhamisi asubuhi, kwenye kikao cha Baraza Kuu, kisio rasmi, walikusanyika wataalamu wa kimataifa walioshiriki kwenye majadiliano yenye hamasa kuu, kuzingatia ile rai ya miaka ya nyuma ya kukomesha kile kilichotafsiriwa na wajumbe wa UM kama ni "kiharusi cha kimataifa" katika kukabili maovu na ukatili unaofanyiwa raia, ndani ya taifa, wakati wenye mamlaka wanaposhindwa kuwapatia raia hawa ulinzi na hifadhi wanayostahiki.

Uwajibikaji wa taifa kulinda raia ni wazo linaloungwa mkono na Pillay

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay ametoa taarifa maalumu iliochangisha maoni ziada kuhusu mjadala unaofanyika wiki hii, hapa Makao Makuu, kuzingatia suala la "Wajibu wa Jumuiya ya Kimataifa Kulinda Raia".

Hali ya wasiwasi Usomali imekwamisha, kwa muda, huduma za kiutu

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR), kwa kupitia msemaji wake Geneva, leo limeripoti kwamba muongezeko wa hali ya wasiwasi katika Usomali unazidisha ugumu wa uwezo wa watumishi wanaohudumia misaada ya kiutu kuwafikia waathirika wa karibuni wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

'Juhudi ziada zahitajika kukomesha uhamisho wa mabavu Uganda Kaskazini', aonya mtetezi wa IDPs

Walter Kaelin, Mjumbe Maalumu wa KM juu ya Haki za Kibinadamu kwa wahamiaji wa ndani ya nchi (IDPs) amenakiliwa akisema ameingiwa moyo na kufurahika kwa "maendeleo aliyoyashuhudia kuhusu utekelezaji wa mahitaji ya watu waliong\'olewa makazi, kwa sababu ya mapigano, katika Uganda Kaskazini, ambapo takriban asilimia 80 ya umma huo, unaojulimsha wahamiaji milioni 1.8, wamesharejea vijijini mwao kwa khiyari."

UNHCR ina wasiwasi juu ya madai wanamaji wa Utaliana waliwatendea kusio huruma wahamiaji wa Eritrea

Ron Redmond, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) ameripoti leo hii, kutokea Geneva, ya kuwa watumishi wa UNHCR waliopo Libya, walifanikiwa kufanya mahojiano na watu 82 waliozuiliwa karibuni na manowari za Utaliana, kwenye eneo la bahari kuu liliopo maili za bahari 30 kutoka kisiwa cha Utaliana cha Lampedusa.