Haki za binadamu

Hapa na Pale

KM Ijumanne amemaliza ziara yake katika Jamhuri ya Korea/Korea ya Kusini. Kabla ya kuondoka mji mkuu wa Seoul, KM alizuru madhabahu ya kuomboleza yaliopo hospitali, kumhishimu aliyekuwa Raisi wa Jamhuri ya Korea, Kim Dae-jung, ambaye alifariki siku ya leo.

Watumishi wawili wa UM, miongoni mwa waliouawa na shambulio la kujiangamiza Afghanistan

Watumishi wawili wa UM katika Afghanistan walikuwa miongoni mwa watu saba waliouawa, Ijumanne ya leo, shambulio la bomu la kujitolea mhanga liliotukia katika sehemuya kati ya mji wa Kabul, siku mbili kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa taifa kuteua wawakilishi wa baraza la majimbo na raisi.

UNAMID imeanzisha kitengo maalumu kuchunguza unyanyasaji wa kijinsiya Darfur

Shirika la UM-UA juu ya Ulinzi Amani kwa Darfur (UNAMID) limeripotiwa kuanzisha kitengo maalumu cha polisi kwa makusudio ya kufanya uchunguzi na kudhibiti makosa ya jinai yanayohusika na matumizi ya nguvu na unyanyasaji dhidi ya wanawake, tatizo ambalo linaripotiwa limeselelea kwa wingi katika eneo la Sudan magharibi la Darfur.

'Wahamiaji waliorejea Sudan kusini wakabiliwa na matatizo magumu makwao': IMO

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), ambalo ni miongoni mwa jumuiya za kimataifa zinazoshirikiana kikazi kwa ukaribu zaidi na UM, limewasilisha ripoti mpya iliotolewa Geneva hii leo, inayozingatia hali ya wahamiaji wa ndani ya nchi pamoja na wahamaji wazalendo waliorejea Sudan Kusini kutoka mataifa jirani na kutoka nje.

UNHCR kuhamisha tena wahamiaji wa Dadaab, Kenya

Andrej Mahecic, msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) aliripoti leo kutoka Geneva kwamba taasisi yao imeanzisha rasmi, wiki hii, operesheni za kuwahamisha wahamiaji wa Usomali 12,900 kutoka kambi ya Dadaab, iliosongamana watu kupita kiasi, na kuwapeleka wahamiaji kwenye kambi ya makaazi ya muda ya Kakuma, iliopo kaskazini-magharibi nchini Kenya.

Waathirika wa chuki za wageni Afrika Kusini wanasema 'bora usalama badala ya anasa za maisha'

Taarifa ya Ofisi ya UM juu ya Huduma za Dharura (OCHA) iliotolewa wiki hii ilielezea mvutano uliozuka kwenye kambi ya makazi ya muda ya Bluewater, katika mji wa Cape Town ambapo wanaishi wahamiaji 396 ambao mnamo mwezi Mei 2008 walifukuzwa kwenye mastakimu ya muda kwa sababu ya tukio liliodaiwa kuwakilisha chuki za wazalendo dhidi ya wageni.

Sheria za kiutu za kimataifa ziliharamishwa Ghaza, imeripoti UM

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay leo ametangaza ripoti yenye kuonyesha kulifanyika uharamishaji wa hali ya juu wa sheria ya kiutu ya kimataifa pamoja na ukiukaji wa haki za binadamu, uliotukia baina ya tarehe 27 Disemba 2008 hadi Januari 18, 2009 katika eneo liliokaliwa la WaFalastina katika Tarafa ya Ghaza.

Uhamisho wa mabavu wa raia katika Port Harcourt, Nigeria waitia wasiwasi UM

Raquel Rolnik, mtaalamu huru wa UM anayetetea haki za umma kupata makazi, ameripoti kutoka Geneva kuingiwa wasiwasi juu ya taarifa alizopokea za kuhamishwa kwa nguvu mamia elfu ya raia waliopo katika Bandari ya Harcourt (Port Harcourt), Nigeria ikiwa miongoni mwa vitendo vya utekelezaji wa sera za serikali za kufufua upya miji.

KM alaumu kifungo ziada cha Aung San Suu Kyi kutoka mahakama ya Myanmar

KM Ban Ki-moon amelaumu uamuzi wa mahakama ya Myanmar, wa kutoa adhabu ziada ya kifungo cha nyumbani cha miezi 18, kwa kiongozi mpinzani na mpokezi wa Tunzo ya Amani ya Nobel, Aung San Suu Kyi.

Dawa ya chanjo kutibu A/H1N1 ni salama kutumiwa, imethibitisha WHO

Shirka la Afya Duniani (WHO) leo limetoa taarifa maalumu inayokana madai yasio msingi, yalioenezwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa, juu ya usalama dhaifu wa zile dawa za chanjo kinga dhidi ya maambukizo ya janga la homa ya mafua ya aina A/H1N1.