Haki za binadamu

Mkurugenzi wa taasisi ya ICGLR azungumza na Redio ya UM juu ya shughuli za shirika lao

Siku ya leo, Ijumatatu tarehe 21 Septemba, ofisi za UM za Makao Makuu zimefungwa rasmi kwa sababu ya Siku Kuu ya Eid al Fitr. Kwa hivyo, badala ya taarifa za habari za kila siku, leo tumekuandalieni kipindi maalumu kuhusu shughuli za Taasisi ya Kimataifa juu ya Masuala ya Kanda ya Maziwa Makuu (ICGRL) yenye makao yake rasmi mjini Bujumbura, Burundi. Makala hii itaongozwa na mimi AWK.

Haki za wahamaji kwenye vizuizi vya idara za uhamiaji zinahitajia marekibisho, anasema Pillay

Alkhamisi mjini Geneva, Baraza la Haki za Binadamu, kwenye pambizo za kikao chake cha mwaka, iliandaa warsha maalumu kuzingatia kwa kina, masuala yanayohusu haki za wahamiaji na wahamaji wanaowekwa kwenye vituo vya kufungia watu vya idara za uhamiaji, haki ambazo katika miaka ya karibuni zilionekana kukiukwa kihorera na mataifa pokezi ya wahamaji.

Kamishna wa Haki za Binadamu ashtushwa na shambulio la kwenye kambi ya wahamiaji wa ndani Yemen

Kamishna Mkuu wa Ofisi ya UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay ametoa taarifa maalumu Ijumaa ilioleza kusumbuliwa sana na taarifa za watu walioshuhudia shambulio la ndege za Yemen, liliotukia tarehe 16 Septemba, kwenye kambi ya muda ya raia waliokimbia mapigano baina ya vikosi vya serikali na waasi wa kundi la Al Houthi, tukio ambalo limesababisha darzeni kadha za vifo vya wahamiaji hawo wa ndani ya nchi.

Kutoruhusu wahamiaji waliokwama baharini kuingia nchini kwaharamisha sheria ya kimataifa, ameonya Pillay

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay kwenye hotuba aliotoa Ijumanne mbele ya wajumbe waliohudhuria kikao cha Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, aliwashtumu vikali wale wenye mamlaka pamoja na manahodha wa meli kadha wanaoharamisha sheria za kimataifa wanapowakatalia kuwachukua wale wahamiaji walioachwa kutangatanga baharini.

Angelina Jolie ashtushwa na hali ngumu kwenye kambi ya wahamiaji wa Usomali mipakani Kenya

Angelina Jolie, msanii maarufu wa michezo ya sinema na Balozi Mfadhili wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) alifanya ziara ya siku moja, mnamo mwisho wa wiki iliopita, katika kambi ya wahamiaji ya Dadaab, iliopo kwenye mpaka kati ya Kenya na Usomali.

Baraza la Haki za Binadamu laanzisha kikao cha kawaida Geneva

Baraza la Haki za Binadamu leo limeanza rasmi kikao chake cha kawaida cha kumi na mbili mjini Geneva. Mkutano ulianza kwa majadiliano ya hadhi ya juu ambapo wawakilishi wa Sri Lanka, Marekani na Thailand walihutubia.

Mwathirika wa mateso ya vita katika JKK azungumzia maafa aliopata na msaada anaotoa kihali kwa waathirika wengine

Mnamo mwanzo wa mwezi Septemba UM uliwakilisha ripoti mbili muhimu, zilizochapishwa na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu na pia kutoka Shirika la Ulinzi Amani la UM katika JKK (MONUC).

NKM atoa mwito wa utendaji dhidi ya udhalilishaji wa wanawake

Kwenye mkutano wa mawaziri kuzingatia masuala ya udhalilishaji na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake, unaofanyika kwenye mji wa Roma, Utaliana, hii leo, NKM Asha-Rose Migiro aliwaambia wajumbe wa kimataifa waliohudhuria kikao hicho ya kuwa madhila ya kutumia mabavu dhidi ya wanawake yaliongezeka zaidi mnamo mwaka uliopita, kwa sababu ya kuporomoka kwa shughuli za soko la fedha la kimataifa.

Ripoti za UM zinasema, inayumkinika makosa ya vita yalitendeka katika JKK

Ripoti mbili zilizotayarishwa bia na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu pamoja na Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC), na kuwasilishwa siku ya leo, zinasema inayumkinika vitendo vya makosa ya jinai ya vita, vikichanganyika na uhalifu dhidi ya utu, viliendelezwa kwenye eneo la mashariki la JKK.

Naibu Katibu Mkuu Asha-Rose Migiro anasailia miaka miwili ya utendaji kazi katika UM

Dktr Asha-Rose Migiro, raia wa Tanzania, alianza kazi rasmi ya NKM wa UM mnamo tarehe mosi Februari 2007. Alikuwa ni NKM wa tatu kuteuliwa kuchukua nafasi hii tangu ilipoanzishwa rasmi katika 1997.