Haki za binadamu

UNHCR kuhamisha tena wahamiaji wa Dadaab, Kenya

Andrej Mahecic, msemaji wa Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) aliripoti leo kutoka Geneva kwamba taasisi yao imeanzisha rasmi, wiki hii, operesheni za kuwahamisha wahamiaji wa Usomali 12,900 kutoka kambi ya Dadaab, iliosongamana watu kupita kiasi, na kuwapeleka wahamiaji kwenye kambi ya makaazi ya muda ya Kakuma, iliopo kaskazini-magharibi nchini Kenya.

Waathirika wa chuki za wageni Afrika Kusini wanasema 'bora usalama badala ya anasa za maisha'

Taarifa ya Ofisi ya UM juu ya Huduma za Dharura (OCHA) iliotolewa wiki hii ilielezea mvutano uliozuka kwenye kambi ya makazi ya muda ya Bluewater, katika mji wa Cape Town ambapo wanaishi wahamiaji 396 ambao mnamo mwezi Mei 2008 walifukuzwa kwenye mastakimu ya muda kwa sababu ya tukio liliodaiwa kuwakilisha chuki za wazalendo dhidi ya wageni.

Sheria za kiutu za kimataifa ziliharamishwa Ghaza, imeripoti UM

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay leo ametangaza ripoti yenye kuonyesha kulifanyika uharamishaji wa hali ya juu wa sheria ya kiutu ya kimataifa pamoja na ukiukaji wa haki za binadamu, uliotukia baina ya tarehe 27 Disemba 2008 hadi Januari 18, 2009 katika eneo liliokaliwa la WaFalastina katika Tarafa ya Ghaza.

Uhamisho wa mabavu wa raia katika Port Harcourt, Nigeria waitia wasiwasi UM

Raquel Rolnik, mtaalamu huru wa UM anayetetea haki za umma kupata makazi, ameripoti kutoka Geneva kuingiwa wasiwasi juu ya taarifa alizopokea za kuhamishwa kwa nguvu mamia elfu ya raia waliopo katika Bandari ya Harcourt (Port Harcourt), Nigeria ikiwa miongoni mwa vitendo vya utekelezaji wa sera za serikali za kufufua upya miji.

KM alaumu kifungo ziada cha Aung San Suu Kyi kutoka mahakama ya Myanmar

KM Ban Ki-moon amelaumu uamuzi wa mahakama ya Myanmar, wa kutoa adhabu ziada ya kifungo cha nyumbani cha miezi 18, kwa kiongozi mpinzani na mpokezi wa Tunzo ya Amani ya Nobel, Aung San Suu Kyi.

Dawa ya chanjo kutibu A/H1N1 ni salama kutumiwa, imethibitisha WHO

Shirka la Afya Duniani (WHO) leo limetoa taarifa maalumu inayokana madai yasio msingi, yalioenezwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa, juu ya usalama dhaifu wa zile dawa za chanjo kinga dhidi ya maambukizo ya janga la homa ya mafua ya aina A/H1N1.

Wahamiaji wa Usomali Kenya kufadhiliwa na UNHCR msaada wa $20 milioni

Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) kwenye ziara yake rasmi nchini Kenya wiki hii alitangaza kwamba watafadhilia msaada wa dola milioni 20 kutumiwa kukidhi mahitaji ya wahamiaji wa Usomali pamoja na jamii ya wenyeji wao waliopo Kenya

Kamishna wa Haki za Binadamu aingiwa wahka na ripoti za fujo Nigeria

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay, ametangaza hii leo kutoka Geneva ya kwamba ana wahka mkubwa kuhusu ripoti alizopokea, juu ya taathira za kufumka kwa vurugu ikichanganyika na hali mbaya ya raia iliotanda majuzi katika eneo la Nigeria kaskazini, kufuatia mashambulio ya wafuasi wa kundi la kidini linaloitwa ‘Boko Haram\'.