Majuzi katika mji wa Dakar, Senegal kulifanyika kikao maalumu cha ushauriano, kilichoandaliwa na Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) pamoja na jumuiya 30 za kiraia, kwa lengo la kubuni miradi itakayohakikisha umma huwa unapatiwa uwezo wa kujikinga na UKIMWI, na kupata huduma zinazoridhisha za matibabu, pamoja na uangalizi na misaada ya fedha inayohitajika kutekeleza huduma hizo za afya kwa waathirika.