Olivier De Schutter, Mkariri Maalumu juu ya haki ya chakula ameiambia Kamisheni ya UM juu ya Maendeleo Yanayosarifika kwamba umma wa kimataifa unalazimika kuandaa, kidharura miradi madhubuti itakayoimarisha na kudumisha mifumo ya kuzalisha chakula kwa wingi, kwenye mazingira ya ulimwengu wa sasa, mazingira yaliokabiliwa na madhara kadha wa kadha yanayochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa na kupungua kwa maliasili duniani.