Haki za binadamu

Hapa na pale

Shirika la Haki za Wafanyakazi wa Kimataifa (ILO) limetoa ripoti mpya yenye kuzingatia ‘Mwelekeo wa Ajira Duniani kwa 2008’ na kuonya kwamba kwa kulingana na takwimu za ILO watu milioni 5 watanyimwa ajira mwaka huu kwa sababu ya kutanda kwa misukosuko ya uchumi, ambayo huchochewa na machafuko kwenye soko la mikopo, pamoja na mfumko wa bei za mafuta katika soko la kimataifa.~

Mjumbe Mpya wa KM katika JKK akutana na viongozi kuzungumzia amani

Alan Doss, Mjumbe Maalumu mpya wa Katibu Mkuu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) amekutana majuzi na Raisi Joseph Kabila pamoja na maofisa wa serikali mjini Kinshasa ambapo walizingatia kipamoja masuala yanayohusu shughuli za ulinzi wa amani katika DRC.

Mashirika ya UM yaendelea kuhudumia misaada ya kiutu Kenya

UM na mashirika yake mbalimbali yaliopo Kenya yanashiriki kwenye huduma kadha wa kadha za kukidhi mahitaji ya umma ulioathiriwa na machafuko yaliyofumka karibuni nchini Kenya baada ya uchaguzi kumalizika. Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) misaada hii hugaiwa na kuenezwa kwenye maeneo muhitaji na mashirika ya UM, mathalan UNHCR, WFP na UNICEF, hususan katika lile eneo la Kaskazini la Mkoa wa Bonde la Ufa/Northern Rift Valley.