Haki za binadamu

Ripoti ya UM inasema ukamataji wa kihorera Sudan umetanda nchi nzima

Ripoti ya Ofisi ya Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu (OHCHR) kuhusu Sudan, iliowasilishwa rasmi leo Ijumaa mjini Geneva, inasema ukamataji wa kihorera wa raia na uwekaji kizuizini kwa watu wasio hatia, umezagaa katika sehemu nyingi za nchi, na ni vitendo ambavyo ripoti ilisema hufungamana na ukiukaji wa haki za binadamu unaoambatana na watu kuteswa na vitendo vyengine vya uoenevu na unyanyasaji.

Tume ya UM inajiandaa kuchunguza kesi 500 za watu waliotoroshwa kimabavu

Tume ya Utendaji ya UM kuhusu Watu Waliotoroshwa na Kupotezwa Kimabavu inajitayarisha kufanya mapitio ya kesi 500 ziada za waathiriwa waliotoweka kufuatia ripoti ilizopokea kutoka nchi wanachama 34.

Mtaalamu Huru wa UM juu ya Haki za Binadamu ahadharisha mateso yamepamba vizuizini Guinea-Bissau

Manfred Nowak, Mkariri Maalumu wa UM juu ya Mateso na adhabu nyengine katili zinazodhalilisha utu, baada ya kumaliza ziara yake katika taifa la Guinea-Bissau, aliwaambia waandishi habari ya kwamba raia wanaojikuta kwenye vizuizi vya polisi katika taifa hilo [mara nyingi] huteswa na kusumbuliwa kwa mpangalio, na wakati huo huo wafungwa huadhibiwa kikatili kabisa, hali ambayo anaamini inasababishwa na kuharibika kabisa kwa mfumo wa sheria katika nchi. Alisema wafungwa wa kisiasa, pamoja na wale watuhumiwa wa uhalifu wa kawaida, wote huteswa na polisi katika Guinea-Bisaau, [pale wanaposhikwa na hulazimishwa] wakubali kukiri makosa bila ushahidi wala kupelekwa mahakamani.~~

Ukumbi mpya wa mikutano umefunguliwa rasmi Geneva kuhishimu haki za binadamu na tamaduni anuwai

KM Ban Ki-moon leo yupo Geneva, Uswiss akihudhuria ufunguzi wa ukumbi wa kisasa wa kufanyia mikutano, uliojengwa upya na kupambwa kwa michoro ya msanii maarufu wa Uspeni anayeitwa Miquel Barcelos.

Kamishna wa Haki za Binadamu ainasihi Israel kukomesha, halan, vikwazo dhidi ya Ghaza

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay Ijumanne ametangaza taarifa, yenye mwito maalumu, wenye kuinasihi Israel kukomesha, haraka iwezekanavyo, vikwazo vyote dhidi ya eneo la Tarafa ya Ghaza.

Mkariri wa Haki za Binadamu ahadharisha dhidi ya hatari ya ubaguzi uliojificha

Ripoti yetu wiki hii inazingatia juhudi za kimataifa kukabiliana na janga la ukabila na ubaguzi wa rangi, hususan kwa wahamaji wanaojikuta kwenye mazingira ya ugenini.~~

Mtaalamu wa Haki za Binadamu anahimiza nchi maskini zisamehewe madeni

Dktr Cephas Lumina, Mtaalamu Maalumu wa UM juu ya Haki za Binadamu juu ya athari za madeni kwa ustawi wa uchumi wa nchi zinazoendelea alinakiliwa kwenye ripoti alioitoa kabla ya Mkutano wa Doha, utakaofanyika katika siku za karibuni, ya kwamba Nchi Wanachama zitakazohudhuria kikao hicho zitalazimika kukamilisha juhudi za pamoja za kupunguza mzigo huo wa madeni.~~

Raisi wa Baraza la Haki za Binadamu anahimiza subira juu ya kazi zake

Raisi wa Baraza la UM juu ya Haki za Binadamu, Martin IHOEGHIAN UHOMOIBHI wa Nigeria alipowasilisha ripoti yake Ijumanne mbele ya Baraza Kuu juu ya kazi ya taasisi anayoiongoza, alitahadharisha wajumbe wa kimataifa wawe na subira kabla ya kutoa maamuzi juu ya namna shughuli za Baraza zinavyotekelezwa, kwa sababu bodi hilo linashuhudia siku za mwanzo za hatua za mabadiliko katika shughuli zake.