Haki za binadamu

Mahojiano na M.Shirika, mwaathiriwa wa kunajisiwa kimabavu JKK

Mnamo mwezi Septemba Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF), kwa ushirikiano na wanaharakati wa Marekani wanaogombania haki za wanawake wa jumuiya isiyo ya kiserikali inayoitwa V-Day, walitayarisha warsha maalumu katika majimbo ya Bukavu na Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) ziliopewa mada isemayo “Wanawake Wavunja Ukimya na Miko ya Kijadi” – tukio ambalo, kwa mara ya kwanza, kihistoria, wale wanawake walionusurika na ajali ovu ya kunajisiwa kimabavu, walipata fursa ya kuelezea mateso yao hayo hadharani. Kitendo hiki kilitaka ujasiri mkubwa, na lengo hasa lilikuwa ni kuwasaidia waathiriwa kuyapunga yale marohani yaliowasumbua kiakili ili waweze kupiga hatua ya kusonga mbele kimaisha.

Mahojiano na L. Sinai, mwaathiriwa wa pili wa mateso ya kijinsiya katika JKK

Mnamo mwezi Septemba Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF), kwa ushirikiano na wanaharakati wa Marekani wanaogombania haki za wanawake wa jumuiya isiyo ya kiserikali inayoitwa V-Day, walitayarisha warsha maalumu katika majimbo ya Bukavu na Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) ziliopewa mada isemayo “Wanawake Wavunja Ukimya na Miko ya Kijadi” – tukio ambalo, kwa mara ya kwanza, kihistoria, wale wanawake walionusurika na ajali ovu ya kunajisiwa kimabavu, walipata fursa ya kuelezea mateso yao hayo hadharani. Kitendo hiki kilitaka ujasiri mkubwa, na lengo hasa lilikuwa ni kuwasaidia waathiriwa kuyapunga yale marohani yaliowasumbua kiakili ili waweze kupiga hatua ya kusonga mbele kimaisha.~

Waathiriwa walionajisiwa kimabavu wadai kurejeshewa haki katika JKK

Hivi karibuni Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF), likijumuika na wanaharakati wa Marekani wanaogombania haki za wanawake wanaowakilisha kundi linalojulikana kwa umaarufu kama Jumuiya ya V-Day, walitayarisha warsha mbili muhimu za pamoja, katika miji ya Goma na Bukavu. Kauli mbiu ya mkusanyiko huo ilikuwa na mada isemayo “Wanawake Wavunja Ukimya na Miko” – ambapo kwa mara ya kwanza, kihistoria, wale wanawake walionusurika na janga ovu la kunajisiwa kimabavu, walipata fursa ya kujieleza, hadharani, mbele ya kadamnasi ya raia, juu ya mateso waliopata kutokana na udhalilishaji wa kijinsia.

Tume juu ya tukio la Beit Hanoun yawakilisha ripoti katika HRC

Hii leo mjini Geneva kwenye ukumbi wa Baraza la Haki za Binadamu (HRC), Askofu Mkuu wa Afrika Kusini Desmond Tutu aliwakilisha ripoti ya mwisho juu ya matokeo ya uchunguzi waliofanya tume aliyoiongoza, ya hadhi ya juu, kuhusu shambulio la mwezi Novemba 2006 kwenye eneo la Wafalastina liliokaliwa kimabavu na Israel la Beit Hanoun, liliopo katika Tarafa ya Ghaza, ambapo raia 19 waliuawa na mizinga ya wanajeshi wa Israel.

Haki za Binadamu zinazorota Sudan, adai Sima Samar

Baraza la Haki za Binadamu Geneva leo limezingatia ripoti iliowasilishwa na Sima Samar, Mkariri Maalumu juu ya hali ya haki za binadamu katika Sudan. Alisema alipowasilisha ripoti, ya kwamba hali nchini humo bado inakabiliwa na vizingiti kadha wa kadha vyenye kutatanisha utekelezaji unaofaa wa haki za binadamu Sudan.

ICRC inasema Usomali inahitajia misaada ya kihali

Marcel Izard, Msemaji wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (ICRC) aliwaambia waandishi habari leo Geneva kwamba hali katika Usomali bado inaendelea kuharibika na shirika lao linajaribu kuhudumia umma muathiriwa mahitaji yao ya kimsingi.~

Siku ya Kimataifa ya Demokrasia

Leo asubuhi kwenye ukumbi wa Baraza Kuu la UM, katika Makao Makuu, kuliadhimishwa, kwa mara ya kwanza Siku ya Kimataifa ya Demokrasia, ambapo kulifanyika mapitio juu ya hali ya mfumo wa kidemokrasi ilivyo sasa hivi duniani.

Waathiriwa walionajisiwa kimabavu JKK wavunja ukimya wa mateso yao hadharani

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) likijumuika na kundi la wanaharakati wa Marekani wanaogombania haki za wanawake, wa kutoka Jumuiya ijulikanayo kama V-Day, wametayarisha warsha mbili muhimu katika miji ya Goma na Bukavu, ikiwa miongoni mwa kampeni za pamoja kukabiliana na matatizo ya udhalilishaji wa kijinsia katika JKK ambapo, mara nyingi wanawake hukamatwa kimabavu na kunajisiwa.

Coomaraswamy anasihi hifadhi bora kwa watoto walionaswa kwenye mazingira ya uhasama

Mjumbe Maalumu wa KM juu ya Hifadhi ya Mtoto katika Mazingira ya Vita na Mapigano, Radhika Coomaraswamy Ijumanne alihutubia Baraza la Haki za Binadamu linalokutana mjini Geneva, ambapo alikumbusha watoto karibu 300,000 walilazimishwa kujiunga, kama wapiganaji, na makundi kadha ya wanamgambo yanayoshiriki kwenye vurugu na uhasama katika sehemu kadha wa kadha za dunia.

UM umeitisha mjadala maalumu kusikiliza hisia na maoni ya waathiriwa wa ugaidi duniani

Hii leo, kwenye Makao Makuu ya UM mjini New York, kumeanzishwa mjadala maalumu wa kihistoria, ulioandaliwa na KM Ban Ki-moon mwenyewe, ambao umewakusanyisha waathiriwa wa vitendo vya ugaidi kutoka sehemu kadha za kimataifa na kuwapatia fursa ya kuelezea hisia zao juu ya misiba waliopitia, kwa madhumuni ya kuwakilisha taswira ya kiutu kwa waathiriwa wa janga la ugaidi duniani.