Haki za binadamu

Uchaguzi wa uraisi Zimbabwe sio halali, anasema KM

KM Ban Ki-moon, kwenye taarifa iliotolewa kwa kupitia msemaji wake, amelaumu na kushtumu matokeo ya uchaguzi wa uraisi uliofanyika Zimbabwe mwisho wa wiki iliopita, uchaguzi ambao alisisitiza umekosa uhalali chini ya hsreia ya kimataifa.

UNESCO kuanzisha muungano wa manispaa za kimataifa dhidi ya ubaguzi

Kwenye Warsha juu ya Haki za Binadamu unaofanyika Nantes, Ufaransa kulianzishwa na Shirika la UM juu ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jumuiya mpya ya muungano wa miji ya kimataifa, itakayoshirikisha manispaa za miji hiyo kwenye juhudi za kuandaa mitandao itakayoshughulikia juhudi za kuimarisha sera bora za kupiga vita kipamoja ubaguzi wa rangi na, kutunza tabia ya kuheshimiana, kwa kupendekeza kusuluhisha matatizo ya ubaguzi wa rangi kwa mazungmumzo badala ya adhabu, na kuhakikisha pia tamaduni tofauti au tabia anuwai zilizoselelea kwenye maeneo yao zinaruhusiwa kustawi bila ya pingamizi. ~

Haki Zimbabwe lazima itimiziwe waathiriwa wa vurugu la uchaguzi, anasihi Arbour

Louise Arbuor, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu amenakiliwa akisema kwamba angependa kuona haki inakamilishwa Zimbabwe, mapema iwezekanvyo, dhidi ya wale watu walioshiriki kwenye kampeni za kisiasa, zilizokiuka maadili ya kiutu, na zilizochafua utaratibu wa kidemokrasia nchini humo, kufuatilia duru ya kwanza ya uchaguzi wa taifa mnamo Machi 29 (2008).~

Nchi wanachama zahimizwa kuidhinisha mkataba dhidi ya mateso

Tarehe ya leo, Juni 26, inaheshimiwa kuwa Siku ya Kimataifa ya Ushikamano na Waathiriwa wa Mateso, siku ambayo KM aliitumia kutoa mwito unayoyahimiza Mataifa Wanachama wa UM kuidhinisha haraka Mkataba dhidi ya Mateso, na pia kuridhia Itifaki ya Khiyari ya Mkataba huo ambao hujumuisha pendekezo la kuchunguza, bila ya vizuizi, vituo vya kufungia watu vya kitaifa na kimataifa, ili kutathminia utekelezaji wa haki za wafungwa. ~

Nowak ainasihi Zimbabwe kusitisha mateso na fujo

Manfred Nowak, Mkariri Maalumu wa UM juu ya Masuala ya Mateso na Vitendo Katili vya Kuadhibu na Kudhalilisha Utu ametoa mwito kwa Serikali ya Zimbabwe na jumuiya ya kimataifa wajumuike kipamoja, kidharura, kufanya kila wawezalo kusitisha haraka fujo na vitendo vya mateso nchini humo dhidi ya raia.

Wataalamu wa haki za binadamu wanalaani kampeni ya kung'oa watu makwao kimabavu Zimbabwe

Kadhalika, kundi la wataalamu maalumu wa Kamisheni ya UM juu ya Haki za Bindamau hii leo wamewasilisha ripoti ya shirika iliosisitiza kuingiwa na wahaka mkubwa na khofu juu ya hali na usalama wa watu 200,000 waliongo\'lewa mastakimu na makazi katika mji wa Harare na katika sehemu nyengine 29 nchini Zimbabwe.

UM inasema wanawake wanahitajia kinga imara dhidi ya mateso

Taasisi za UM zinazoshughulikia juhudi za kimataifa za kukomesha mateso na kusaidia waathiriwa wa janga hili, zimetoa taarifa muhimu yenye kusisitiza kwamba walimwengu bado watahitajia kuchangisha bidii zao kwa wingi zaidi ili kufanikiwa "kuwapatia kinga na hifadhi madhubuti kila mwanadamu mstahiki dhidi ya mateso" licha ya kuwepo ulimwenguni kwa vyombo kadha wa kadha vya sheria ya kimataifa vinavyoharamisha janga hilo.

UM kukabidhiwa matokeo ya kura ya maoni ya kimataifa dhidi ya kutesa

Matokeo ya ripoti ya kura ya maoni ilioendelezwa kwemye mataifa 19 mbalimbali duniani na taasisi ijulikanayo kama WorldPublicOpinion.org yamekabidhiwa UM mapema wiki hii.

BU kushtumu fujo na utumiaji mabavu Zimbabwe

Ijumatatu usiku, Baraza la Usalama liliafikiana, kwa kauli moja, kushtumu kampeni ya utumiaji mabavu inayoendelezwa na wenye madaraka Zimbabwe, dhidi ya wapinzani wa kisiasa, na pia kulaani vitendo vya Serikali ambavyo inaripotiwa huwanyima wapinzani haki ya kuendeleza kampeni huru za uchaguzi. Kwenye taarifa iliotolewa baada ya majadiliano ya faragha katika Baraza la Usalama, Raisi wa mwezi Juni wa Baraza, Balozi Zalmay Khalilzad wa Marekani alisema wajumbe wa Baraza wanaamini fujo iliotanda sasa hivi Zimbabwe, ikichanganyika na vikwazo dhidi ya vyama vya upinzani, ni hali ambayo uchaguzi ulio huru na wa haki hauwezekani kufanyika abadan, uchaguzi ambao umetayarishwa ufanyike Juni 27 (2008).

UNHCR inashinikiza mfanyakazi aliotekwa nyara Usomali aachiwe

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kuwa linaendelea kushinikiza, kwa sauti kuu, aachiwe huru yule mfanyakazi wao, Hassan Mohammed Ali, ambaye alitekwa nyara Ijumamosi iliopita kutoka nyumbani kwake katika mji wa Afgooye, kilomita 30 kutoka Mogadishu, na watu wasiojulikana. Kwa mujibu wa UNHCR mateka Ali aliweza kuzungumza kwa simu na aila yake Ijumapili usiku na alisema hali yake ni nzuri; lakini taarifa nyengine ziada yoyote kuhusu mahali alipo na utambulisho wa makundi yaliomtorosha haijulikani. ~