Haki za binadamu

Mjumbe wa AMREF, Tanzania anazungumzia fungamano za haki za binadamu na mahusiano ya kijinsia

Katika wiki ambapo jumuiya ya kimataifa ilikuwa ikiadhimisha miaka 60 ya Azimio la Mwito wa Kimataifa juu ya Haki za Bnadamu, Shirika la Udhibiti wa Idadi ya Watu (UNFPA) liliitisha jopo maalumu, mjini New York kwenye Makao Makuu ya UM, kuzingatia fungamano kati ya haki za binadamu na mahusiano ya kijinsia.

UM unaadhimisha miaka 60 ya utetezi wa Haki za Binadamu

Wiki hii UM uliadhimisha miaka 60 ya kupitishwa kwa Azimio la Mwito wa Kimataifa juu ya Haki za Binadamu, ambayo husherehekewa kila mwaka mnamo tarehe 10 Disemba. ~

KM anatafakaria Azimio la Haki za Binadamu kuadhimisha Siku ya Kimataifa juu ya Haki za Kimsingi

“Hii leo, kwenye Siku ya Kusherehekea Haki za Binadamu, vile vile tunaadhimisha miaka sitini tangu Azimio la Kimataifa juu ya Haki za Binadamu lilipopitishwa.

Utekelezaji wa haki za binadamu kimataifa wahitajia bidii ziada, asema Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu

Jumuiya ya kimataifa pia mwaka huu inaadhimisha waraka muhimu wa kihistoria, unaojulikana kwa umaarufu kama Azimio la Kimataifa juu ya Haki za Binadamu, waraka ambao tarehe ya leo umetimiza miaka 60 tangu kupitishwa na Baraza Kuu.

UM unaadhimisha na kuhishimu Siku ya Kimataifa kwa Watu Walemavu

KM Ban Ki-moon leo asubuhi, kwenye risala alioitoa kuadhimisha Siku ya Kimataifa kwa Watu Walemavu alisema asilimia 80 ya umma huu – inayokadiriwa kujumlisha walemavu milioni 400 ziada – wanaishi katika nchi maskini – na ni wajibu wa serikali zote za nchi wanachama katika UM kukomesha duru ya ufukara na ulemavu.

Kwenye taadhima za Siku ya Kuondosha Utumwa Duniani KM Ban ahadharisha athari za utumwa mamboleo

Mataifa Wanachama wa UM wanaadhimisha Disemba pili kuwa ni Siku Kuu ya Kuondosha Utumwa Duniani.

Baraza la Haki za binadamu lalaani ukiukaji wa haki za kimsingi dhidi ya raia katika JKK

Baraza la Haki za Binadamu, ambalo tangu wiki iliopita lilikutana mjini Geneva, Uswiss kujadilia masuala yanayohusu utekelezaji wa haki za binadamu kwenye eneo la mashariki, katika JKK, leo limetoa taarifa ilioshtumu na kulaani vikali, ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya raia, ulioonekana kuendelezwa kwenye sehemu hizo za nchi katika wiki za karibuni.