Haki za binadamu

UNHCR inasema chuki za wageni Afrika Kusini zawahamasisha wahamiaji wakazi kurudi makwao

UM inashiriki kwenye huduma za kuwasaidia kurejea makwao wageni kadhaa waliong’olewa makazi Afrika Kusini, kwa sababu hawana furaha na maisha wanaoongoza nchini humo kwa sasa, hasa baada ya kufumka vurugu la chuki za wageni katika mwezi Mei lilioenea nchini humo kwa wakati huo.

UM inawakumbuka waliopotea kimabavu duniani

Tume ya Utendaji ya UM juu ya Watu Waliotoweka Kimabavu itaadhimisha miaka 25 ya Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka Waliotoweka Duniani. Siku hiyo huadhimishwa kila mwaka mnamo tarehe 30 Agosti.

OHCHR imeshtumu utumiaji nguvu dhidi ya IDPs katika Darfur

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu imetoa taarifa mjini Geneva Ijumaa ilioshtumu vikosi vya usalama vya Sudan kwa kutumia nguvu isiowiana na makosa yanayodaiwa kufanyika katika kambi ya wahamiaji wa ndani ya Kalma, katika Darfur.

UM washiriki kwenye mkutano wa Afrika kupiga vita ubaguzi wa rangi

Kuanzia Ijumapili tarehe 24 Agosti (2008) maofisa wa UM pamoja na wawakilishi wa serikali za Afrika na wataalamu kutoka jumuiya za kiraia, hali kadhalika, walikutana kwenye mji mkuu wa Abuja, Nigeria kwenye kikao cha siku tatu, kuzingatia masuala yanayohusu ukabila, ubaguzi wa rangi, chuki za wageni na mifumo mengineyo inayofungamana na utovu wa kustahamiliana.

Wanaotengua haki za ilimu wapewe adhabu, anasihi Villalobos

Vernor Munoz Villalobos, Mkariri Maalumu wa UM juu ya Haki za Kupata Ilimu ametoa taarifa maalumu Geneva inayopendekeza wale wanaoshambulia walimu, wanafunzi na maskuli wakamatwe na wapelekwe mahakamani kukabili haki na kuhukumiwa adhabu kali.

UM unasisitiza mazeruzeru watekelezewe haki zao halali halan

Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) limenasihi kwenye ripoti iliotolewa karibuni ya kwamba ni muhimu kwa UM kujihusisha, kikamilifu, katika kugombania haki za mazeruzeru duniani. Wiki iliopita UNDP ilisimamia warsha maalumu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) kuzingatia namna ya kuwasaidia mazeruzeru kujihudumia kimaisha, fungu la raia ambao kikawaida hukabiliwa na ubaguzi wa kila aina wa kijamii dhidi yao nchini.

UM wabainisha wahka juu ya maamuzi ya Mahakama ya Kukabili Ugaidi Sudan

Mwakilishi Maalumu wa KM kwa Sudan, Ashraf Qazi, Alkhamisi alitoa taarifa rasmi iliotathminia hukumu ya kifo iliopitishwa karibuni na Mahakama ya Kukabili Ugaidi ya Sudan, dhidi ya wafuasi 30 wa kundi la waasi la JEM, taarifa ambayo ilibainisha wasiwasi wa UM juu ya uamuzi ambao ilisema haulingani na viwango vya sheria ya kimataifa.

Mwanaharakati wa haki za binadamu Kenya azungumzia ushirikiano na UM

Mnamo mwanzo wa wiki mwanaharakati anayepigania haki za binadamu Kenya, James Maina Kabutu alikuwa na kikao maalumu cha ushauri na Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF). Mwanaharakati huyu anawakilisha mashirika mawili ya kiraia yajulikanayo kama Hema la Katiba na Bunge la Mwananchi.