Haki za binadamu

Watesaji wasiruhusiwe kukwepa sheria kwa uhalifu wao:UN

Katika siku ya kimataifa ya kusaidia waathirika wa utesaji Umoja wa Mataifa unataka hatua Madhubuti zichukuliwe ili kuhakikisha watesaji wanahukumiwa kutokana na uhalifu huo.

Tuzo ya mshindi wa Nobel yauzwa dola milioni 103.5 fedha kugawanywa na UNICEF

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Dmitry Muratov ambaye alipiga mnada medali yake ya dhahabu ili kuchangisha fedha kwa ajili ya wakimbizi watoto Juni 20, 2022 ameiambia Idhaa ya Umoja wa Mataifa kwamba Kitendo cha medali yake kuvunja rekodi kwa kuuzwa dola milioni 103.5 kimethibitisha kwamba "wakati mwingine ubinadamu unaweza kuja pamoja, na kuoyesha mshikamano".

Baada ya kukatwa vidole Iran, wafungwa hatihati kukatwa mkono mzima

Wakati Iran ikiwa katika harakati za kuwakata vidole vyote vya mkononi wafungwa 8 baada ya kupatikana na hatia ya wizi, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, OHCHR imeelezea wasiwasi wake huku ikitaka serikali ya Iran ifutilie mbali mpango huo.

Hivi ndivyo tunavyopaswa kusaidia wathaarika wa unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo ya vita

Unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo ya vita ni moja ya mbinu ya kivita na ukandamizaji ambayo imeathiri idadi kubwa ya watu, kuharibu maisha yao na kuvunja jamii kwakuwa waathirika wa unyanyasaji huo hubeba mzigo mkubwa wa unyanyapaa, kuathirika kisaikolojia na mara nyingi jamii kuwatupia lawama huku wahalifu mara chache huchukuliwa hatua kwa matendo yao.

Kauli za chuki ni hatari kwa kila mtu: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kauli za chuki ni hatari kwa watu wote na kila mtu anao wajibu wakuzuia kauli hizo katika jamii.

Watoto wangu hawatemewi tena mate, nashukuru UN- Mama Kasereka

“Nilianza kufanya shughuli za kujiuza mwili nikiwa na umri mdogo”, kwa masikitiko makubwa anaanza kueleza ambaye alipoteza wazazi akiwa mdogo na kukulia katika mazingira ya vita nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC.

Tanzania: UN yahofia ghasia kutokana na madai ya kumegwa kwa ardhi ya asili ya wamasai

Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameeleza hofu yao juu ya madai ya kuendelea kumegwa kwa ardhi ya asili ya wamasai huko Loliondo kaskazini mwa Tanzania.

Taarifa za awali zadokeza uhalifu wa kivita na ukiukwaji wa haki za binadamu Ukraine- Kamisheni 

Kamisheni iliyoundwa na Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu kuchunguza madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu na sheria za kimataifa za kibinadamu nchini Ukraine imetoa ripoti ya ziara yake ya kwanza nchini Ukraine na kusema ingawa haiko katika nafasi ya kuwa na vigezo vya kisheria au matokeo kamilifu, taarifa za awali zinadokeza kuweko kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na sheria za kimataifa za kiutu. 

Ukiukwaji wa haki za binadamu unaendelea Myanmar aonya Bachelet

Hali ya haki za kibinadamu nchini Myanmar imeendelea kuzorota kwa kasi, amesema Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, Michelle Bachelet akizungumza mjini Geneva Uswisi hii leo kwenye mkutano wa 50 wa Baraza la Haki za binadamu.  

Chanya na Hasi za miaka 15 ya mkataba wa kimataifa wa haki za watu wenye ulemavu

Mkutano wa 15 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu, CRPD umeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kwa lengo la kutathmini miaka 15 tangu kupitishwa kwa mkataba huo ulioridhiwa na mataifa 185.