Kamishia Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet leo ametoa wito wa haraka kwa nchi kupitisha "ajenda ya mabadiliko ili kung'oa ubaguzi wa kimfumo, kama alivyochapisha ripoti ikitoa mwangaza juu ya ukiukaji wa haki za kiuchumi, kijamii, kitamaduni, kiraia na kisiasa unaowakabili watu wa asili ya Kiafrika kila siku katika mataifa tofauti.”