Ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa malengo ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake miaka 75 ya uwepo wake, kuwa mtetezi mkubwa wa amani na haki za wanadamu kote duniani, nchini Sudan Kusini, mpango wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS umeshirikiana na Jeshi la wananchi wa Sudan Kusini SSPDF kuwapa mafunzo wakufunzi kuhusu kuzuia ukatili wa kingono unaohusiana na mizozo.