Haki za binadamu

Vikwazo dhidi  ya Venezuela ni ‘mwiba’ kwa raia wasio na hatia- Mtaalamu

Mtalaamu maalum wa Umoja wa Mataifa amesema vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Venezuela si jibu la mzozo unaoendelea nchini humo na badala yake vitasababisha njaa na ukosefu wa huduma za matibabu.

Watu sita walifariki dunia kila siku wakivuka Mediteranea kuelekea Ulaya 2018

Watu sita walifariki kila siku mwaka jana wakiwa safarini kuvuka bahari ya Mediterenea kuingia bara Ulaya, safari hiyo ikitajwa kama ni ya hatari zaidi kupitia bahari kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

Uchunguzi lazima ufanyike kufuatia kupasuka kwa bwawa Brazil:UN

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametoa wito wa kufanyika haraka uchunguzi wa kina na huru kufuatia kupasuka kwa bwawa huko Minas Gerais nchini Brazil mnamo Januari 25 mwaka huu , hilo likiwa ni tukio la pili linalohusisha kampuni moja katika kipindi cha miaka mitatu.

 

 

UN inashirikiana na serikali Tanzania kubaini chanzo cha mauaji ya watoto 10 mkoani Njombe

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake kufuatia mauaji ya watoto kumi katika mkoa wa kusini mwa Tanzania wa Njombe  ambako yaelezwa kuwa viungo vya mwili vya watoto hao vilinyofolewa.

Umoja wa Mataifa walaani mauaji ya watoto mkoani Njombe Tanzania.

Umoja wa Mataifa nchini Tanzania umeeleza kusikitishwa kwake na mauaji ya watoto yaliyotokea mkoani Njombe nchini humo.

UN yaelezea kusikitishwa na ukatili unaoshuhudiwa Cameroon

Umoja wa Mataifa umeelezea kusikitishwa na taarifa za ukatili na matumizi ya nguvu yanayofanywa na vikosi vya usalama nchini Cameroon wakati wa maandamano katika siku za hivi majuzi kwenye mji wa Douala.

Waisraeli waliowashambulia wapalestina wawajibishwe-OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR imesikitishwa na vurugu za mashambulizi ya muda mrefu dhidi ya wapalestina ikirejelea shambulizi la hivi karibuni katika kijiji cha Al Mughayyir kilichoko katika ukingo wa magharibi wa mto Jordan.

Makaburi ya pamoja yabainika huko DRC

Zaidi ya makaburi 50 ya pamoja nay a mtu mmoja mmoja yamebainika kwenye eneo la Yumbi, jimbo la Mai-Ndombe nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kufuatia mauaji yaliyoripotiwa kwenye eneo  hilo  katikati ya mwezi uliopita wa Disemba. 

Wakati wa mauaji tuliizoea mikokoteni iliyojaa maiti- Manusura wa mauaji ya wayahudi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia kumbukizi ya kuwaenzi waliopoteza maisha na manusura wa mauaji ya halaiki dhidi ya wayahudi yaliyotokea wakati wa Vita Vikuu vya pili vya dunia ameyaita mauaji hayo kuwa ni ya kikatili na ya kutisha kupindukia. 

Chuki dhidi ya wayahudi yaongezeka, tuchukue hatua: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kumbukizi ya mwaka huu ya mauaji ya halaiki inakuja wakati ambapo kuna ongezeko la chuki dhidi ya wayahudi.