Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein ameonya juu ya janga linaloendelea huko jimbo la Daraa nchini Syria wakati huu ambapo ghasia zinazidi kuongezeka.
Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Myanmar, Yang Lee anatarajia kuanzaziara ya kikazi hapo kesho tarehe 29 kwenye mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka na maeneo mengine ya Cox’s Bazarambako wakimbizi kutoka Myanmar wanaishi katika makazi ya muda.
Vitendo vya unyongaji wa watoto wahalifu vinavyotekelezwa nchini Iran ni kinyume na wajibu wa nchi hiyo kama mwanachama wa mkataba wa haki za watoto na sheria za kimataifa kuhusu haki za kisiasa na kijamii.
Tume maalumu iliyoundwa na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuchunguza visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Burundi imesema mauaji, uteseji, watu kutoweka na ukiukwaji mwingine bado vinaendelea na kuwa ni tishio kubwa kwa hatma ya haki nchini humo.
Naiomba serikali nchini Iraq kuhakikisha kwamba watoto waliozaliwa kutokana na wazai wao kubakwa wakati wa vita kuheshimwana kupewa ulinzi wa kisheria ili wasitengwe na jamii na kunyanyapaliwa.
Wataalam wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameitaka serikali ya Saudi Arabia iwaachilie huru mara moja wanawake wanaharakati waliowekwa ndani katika msako uliofanyika nchini humo hivi karibuni, wakati huu ambapo taifa hilo limeondoa marufuku ya wanawake kuendesha magari.
Mtaalamu maalum wa umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Eritrea, ameelezea wasiwasi wake kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo pamoja na mvutano wa mpaka unaondelea kati ya Eritrea na jirani yake Ethiopia.
Serikali ya Venezuela imeshindwa kuwawajibisha wakiukaji wa kubwa wa haki za vinadamu ikiwemo mauaji, matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji, watu kuswekwa rumande kinyume cha sheria, ukatili na mateso.