Mwigizaji mashuhuri ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Academy ya nchini Marekani, Geena Davis amevitaka vyombo vya habari kuonesha umuhimu wa mwanamke katika jamii ili kufikia lengo la nane la maendeleo ya milenia, ifikapo mwaka 2015.
Kesho Juni 26 ni siku ya kimataifa ya kuwaunga mkono waathirika wa utesaji na mataifa yote yana sheria ambazo zinapinga utesaji na kuufanya kuwa ni kosa.
Jumuiya ya wafanya biashara imetakiwa kushirikiana kujenga misingi ya kimataifa ambayo itaziweka haki za watoto katika jajenda ya juu ya ushirikiano wa jukumu la kimataifa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo ameteua jopo la wataalamu kumshauri kuhusu masuala ya madai ya ukiukaji wa haki za binadamu na sheria wakati wa hatua za mwisho za mgogoro wa Sri Lanka uliomalizika mwaka jana.
Mafanikio na hadhi ya baraza la haki za binadamu vitapimwa sio kwa taarifa inazotoa, idadi ya maazimio inayopitisha bali ni kwa kiasi gani linaweza kuleta mabadiliko katika jamii.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema linazungumza na serikali ya Uingereza kuhusu kurejeshwa kwa nguvu kwa wakimbizi wa Iraq.