Haki za binadamu

ICC kutangaza hati rasmi ya kumshika kiongozi wa CNDP katika JKK

Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) imetoa hati rasmi ya kumkamata Bosco Ntaganda, kiongozi wa jeshi la mgambo la CNDP, baada ya kutuhumiwa, katika siku za nyuma, kuwalazimisha watoto wenye umri mdogo kujiunga na kundi lao na kushiriki kwenye mapigano, hasa katika wilaya ya utajiri mkubwa wa maadini ya Ituri, iliopo mashariki ya JKK; na alituhumiwa kurudia vitendo hivyo pia katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Utumiaji mabavu na vurugu la Zimbabwe kumshtusha Kamishna wa Haki za Binadamu

Ijumapili, Louise Arbour, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu alitoa taarifa maalumu mjini Geneva iliyoelezea kushtushwa sana na ripoti aliyopokea kuhusu kuendelea kwa vitendo vya mabavu na hali ya vurugu katika Zimbabwe kufuatia uchaguzi wa karibuni.

Siku ya UM Kuwakumbuka Waathiriwa wa Utumwa Duniani - Balozi wa Tanzania anasailia maana hakika ya siku hii kwa Afrika

Mnamo tarehe 25 Machi mwaka huu, kwa mara ya kwanza katika historia ya UM, kulifanyika hafla maalumu kwenye Makao Makuu mjini New York, kuheshimu Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka Waathiriwa wa Janga la Utumwa na Biashara ya Utumwa katika Bahari ya Atlantiki.

Mkutano wa Durban unazingatia hifadhi bora dhidi ya utumwa mamboleo

Shirika la Kimataifa juu ya Uhamaji (IOM) limeripoti kukutana katika mji wa Durban, Afrika Kusini waundaji sera kadha wa kadha pamoja na viongozi wa serikali kutoka mataifa ya kusini mwa Afrika, kwa madhumuni ya kuzingatia namna ya kuandaa taratibu za kuwakinga raia wanaotoroshwa na kupelekwa mbali na makwao kuhudumia vibarua haramu, mathalan, umalaya au ajira isio ya kulazimishwa isiokuwa na malipo. Mkutano unatarajiwa kuendelea kwa siku tatu.

Ulimwengu unahitajia msukumo mpya kufyeka ubaguzi, anasihi Arbour

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Louise Arbour Ijumatatu mjini Geneva alihutubia moja ya mfululizo wa vikao kadha vinavyoandaliwa na ofisi yake kutayarisha mkutano mkuu wa mwakani utakaofanya mapitio kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya Mkutano wa Durban wa 2001 uliokusudiwa kukomesha tatizo la ubaguzi duniani. Arbour aliwaambia wataalamu waliohudhuria kikao cha matayarisho waliohudhuria kikao wa kufyeka ya ofisiyamtatu wakati akizungumzia juu ya matayarisho ya mkutano wa kufuatilia Mkutano wa Durban wa 2001 wa kufyeka ubaguzi duniani, ameshtumu kwamba tangu kikao kilipofanyika wingi wa Mataifa Wanachama yalishindwa kukamilisha mapendekezo ya kukomesha sera za ubaguzi wa rangi kwa sababu zifuatazo.~

UNICEF na V-DAY wanashirikiana kufyeka udhalilishaji wa kijinsia katika JKK

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) pamoja na shirika lisio la kiserikali Marekani, ambalo hujulikana kama Shirika la V-Day au Shirika la Siku ya Ushindi, wameanzisha rasmi mjini New Orleans, kampeni ya kukomesha milele karaha ya kunajisi kimabavu wanawake katika JKK. Kampeni hii imekusudiwa kuhakikisha wale watu wanaoendeleza jinai hiyo ovu dhidi ya utu, wanashikwa na kufikishwa mahakamani kukabili haki.

Mabadiliko ya katiba kuisaidia Senegal kumshitaki Rais wa zamani wa Chad

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Louise Arbour ameipongeza Senegal kwa kurekibisha katiba yanchi ili kuziwezesha mahakama kumshitaki aliyekuwa Raisi wa Chad Hissene Habre ambaye ametuhimiwa kutengua vibaya sana haki za binadamu wakati alipokuwa kiongozi wataifa hilo kati ya 1982 hadi 1990.

UNICEF kuipongeza Afrika Kusini kwa sheria mpya inayolinda haki za watoto

Shirika la Mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNICEF) limepongeza utiaji sahihi wa sheria mpya Afrika Kusini iliokusudiwa kulinda na kutunza haki za watoto, kitendo ambacho kilitafsiriwa kupiga \'hatua kuu\' kimaendeleo na kuhakikisha ustawi na hali njema kwa raia vijana nchini humo.

Baraza la Haki za Binadamu laanza mapitio ya haki katika nchi 16

Kikao cha awali cha Tume ya Utendaji ya Baraza la Haki za Binadamu imeanzisha ukaguzi maalumu, utakaoendelea hadi tarehe 18 Aprili, ambapo nchi wanachama 16 zitatathminiwa namna zinavyotekeleza haki za binadamu kwa raia zao. Miongoni mwa mataifa ya Afrika yatakayochunguzwa katika kikao hiki hujumuisha Algeria, Morocco, Tunisia na pia Afrika ya Kusini.

KM Ban apongeza kufanywa sheria ya kimataifa Mkataba wa Haki za Walemavu

KM Ban Ki-moon amepongeza tukio la kihistoria liliojiri Alkhamisi ambapo Mkataba juu ya Haki za Walemavu ulifanywa rasmi kuwa chombo cha sheria ya kimataifa baada ya Ecuador kuwa taifa la 20 kutia sahihi amana ya kuridhia Mkataba huo. Tangu tarehe 30 Machi 2007 nchi 126 zilitia sahihi Mkataba, na nchi 71 pia zimeidhinisha Itifaki ya Hiyari ya Mkataba itayoruhusu watu binafsi pamoja na makundi kuwa na haki ya kusaidiwa kihali.