Haki za binadamu

Wataalamu wa UM walaumu haki za binadamu zinakiukwa Darfur

Wataalamu saba wa tume ya UM wenye dhamana ya kufuatilia namna haki za binadamu zinavyotekelezwa katika jimbo la Sudan magharibi la Darfur wamewakilisha wiki hii ripoti ya muda mjini Geneva mbele ya Halmashauri ya Haki za Binadamu.

MONUC inasema "vikosi vya Serekali DRC vinakiuka haki za binadamu"

Ripoti ya Shirika la UM la Ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (MONUC) juu ya utekelezaji wa haki za binadamu katika Kongo-DRC kwa Julai imeshtumu vikali vitendo vya wanajeshi wa Serekali, baada ya kuthibitisha kwenye uchunguzi wao kwamba vikosi hivyo vimegunduliwa vikiharamisha haki za binadamu nchini kwa mapana na marefu, ambapo wanajeshi wamekutikana wakiua raia kihorera, wakinajisi wanawake kimabavu, na kuendeleza wizi na dhulma, na kunyanganya raia mali zao.

Baraza Kuu lapitisha Mwito wa Kihistoria juu ya Haki za Wenyeji wa Asili

Alkhamisi Baraza Kuu la UM limepitisha azimio la kihistoria lililoelezea haki za kimsingi kwa watu milioni 370 duniani wenye kutambuliwa kama ni wenyeji wa asili. Azimio limeharamisha ubaguzi wote dhidi ya fungu hili la kimataifa ambalo lilikuwa likitengwa kimaendeleo na nchi zao kwa muda mrefu.

UM unaripoti makumi elfu ya wahamaji wa DRC wameamua kusalia Uganda kwa sasa

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti wahamiaji 25,000 hadi 30,000 wa Jamuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambao walikimbilia eneo la Bungana, Uganda kunusuru maisha baada ya mapigano kufumka wameamua kubakia huko mpaka hali ya utulivu itakaporejea Kivu Kaskazini, jimbo linalopakana na Uganda.

Hapa na pale

Tarehe 10 Septemba iliadhimishwa na UM kuwa ni ‘Siku ya Kuzuia Vitendo Karaha vya Kujiua Duniani’, hasa ilivyokuwa takwimu za wataalamu wa kimataifa zimethibitisha kuwa katika kila nukta 30 mtu mmoja huwa anajiua ulimwenguni kwa sababu kadha wa kadha.