Ripoti mpya ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu tishio la ugaidi kutoka kikundi cha ISIL imetaja changamoto tatu ambazo zinaendelea kusababisha kundi hilo kuwa tishio la amani na usalama duniani.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake, UN-Women Phumzile Mlambo-Ngucka ameonyesha kutiwa moyo na harakati za ongezeko la uwakilishi wa wanawake katika mifumo ya kisiasa na michakato yake akisihi hatua zaidi zichukuliwe kuongeza uwakilishi huo.
Katika tukio la kuadhmisha kumbukizi ya kwanza ya waathirika wa vitendo vya ugaidi duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema sasa ni wakati wa kusikiliza wahanga hao akisema kuwa kusikiliza sauti zao na kuongeza msaada kwao na familia zao ni jambo jema kimaadili.
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR, imesema ina wasiwasi kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Cambodia kufuatia ripoti ya kwamba uchaguzi mkuu ulifanyika mwishoni mwa mwezi uliopita bila ushiriki wa chama kikuu cha upinzani cha CNRP kilichofutwa.
Baada ya vuta nikuvute na kutokuwa na uhakika wa ufadhili kwa shirika la Umoja wa Mataifa la misaada kwa wakimbizi wa kipalestina UNRWA, hatimaye kuna matumaini baada ya baadhi ya wahisani kujitokeza kusaidia angalau shule ziweze kufunguliwa mwezi ujao.
Japan ichukue hatua haraka kulinda makumi ya maelfu ya wafanyakazi wanaoripotiwa kudhulumiwawakati wanafanya kazi ya kusafisha mtambo wa nyuklia ulioharibika wa Fukushima Daichi.
Wataalam wa Umoja wa Mataifa wamezitaka mamlaka nchini Urusi zimuachilie huru mara moja na bila masharti Oleg Sentsov, huku wakielezea wasiwasi wao kuhusu hali yake ya kiafya kwa sasa.
Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamekaribisha uamuzi wa mahakama huko California nchini Marekani wa ya kutaka malipo ya fidia ya dola milioni 289 kwa mtu ambaye alipata saratani baada ya kuwa karibu na dawa ya kuulia magugu.
Ripoti ya ofisi ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi nchini Somalia, UNSOM na ile ya haki za binadamu, OHCHR, imeweka bayana ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanyika nchini humo kati ya mwishoni mwa mwka 2016 hadi mwanzoni ma mwaka 2017.
Kamatakamata ya kiholela inayolenga wachapishaji huru na waandishi wa habari nchini Belarus ni alama ya sheria mpya za ukandamizaji dhidi ya vyombo vya habari vya mtandaoni nchini humo.