Haki za binadamu

Choo 1 kwa watu 200 nchini Marekani, ajabu na kweli

Huwezi kuamini lakini nchini Marekani kuwa maskini ni jambo ambalo mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa anasema kunachochewa na dharau na sera za kikatili.

DRC badilisha rasimu ya muswada kuhusu NGOs- UN

Wataalamu maalum wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameihimiza serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC iangalie upya rasimu ya muswada  kuhusu asasi za kiraia, NGOs, yenye lengo la kudhibiti kazi za mashirika hayo.

Wasafirishaji haramu wa binadamu wameua watu 12 Libya manusura wasaidiwa na UNHCR

Watu 12 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya wasafirishaji haramu wa binadamu nchini Libya kuwafyatulia risasi watu 200 waliokuwa wakishikilia mateka wakati walipojaribu kutoroka.