Kundi la wataalamu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ,leo wamekosoa jinsi utawala nchini Thailand unavyotumia sheria za kuwachafulia majina, kuwapaka matote au kuwaharibia hadhi wanaharakati wa kutetea haki za binadamu akiwemo Andy Hall kwa lengo la kumwanyamazisha .