Mimba za utotoni ni changamoto kubwa nchini Tanzania na hususani katika maeneo ya vijijini. Serikali ya nchi hiyo ikishirikiana na wadau mbalimbali wa elimu, ustawi wa jamii na mashirika ya kitaifa na kimataifa kama la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wanaelimisha jamii wakiwemo wasichana wadogo mashuleni athari za mimba hizo.