Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC tarehe 23 mwezi huu, mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC imeonya kuwa yeyote yule nchini humo ambaye atachochea, ama atashiriki katika fujo kwa kuamuru, kutaka ama kuhimiza au kuchangia kwa njia yoyote ile au kutenda makosa yaliyo chini ya mamlaka ya ICC atashtakiwa na kufikishwa mbele ya mahakama.