Haki za binadamu

Mlo wa siku moja tu ni changamoto kwa wakimbizi na wasaka hifadhi Misri.

Shirika  la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR hii leo mjini Geneva Uswisi limesema msaada unaotolewa kwa wakimbizi walioko Misri uko katika wakati mgumu kutokana na kuongezeka kwa wakimbizi wapya huku kukiwa na vyanzo haba vya rasilimali.

Nchini Chad, madarasa ya wasichana pekee yasaidia kupunguza hofu na kuchagiza usawa wa jinsia

Mwalimu amenyanyua mchoro wa msichana barubaru ambaye amegutuka tu na kubaini kuwa amechafua nguo yake kutokana na kupata hedhi ya kwanza akiwa shuleni. Mwalimu huyu anazungumza na wasichana walioko darasani kwenye mji wa Bol nchini Chad.

Hatuwezi kufikia SDG’s bila kuwajumuisha wahamiaji:Espinosa

Miezi mitatu baada ya kupitishwa kwa mkataba wa kimataifa kwa ajili ya uhamiaji salama, wa mpangilio na wa halali  mjini Marrakesh Morocco, leo  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linajadili utekelezaji wa mkataba huo.

Mamilioni wanufaika na muamko wa kutokomeza kutokuwa na utaifa Afrika Magharibi-UNHCR

Mamilioni ya watu wamekwepa kutokuwa na utaifa Afrika Magharibi kufuatia mataifa mengi kudhamiria kuhakikisha kuwa kila mtu anapata utaifa ifikapo mwaka 2024 kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

UAE mwachieni huru Alia Abdulnour aishi siku zake za mwisho akiwa huru-Wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

Watalaamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa hii leo mjini Geneva Uswisi wamezisihi Falme za nchi za Kiarabu UAE kumwachia huru Alia Abdulnour, mwanamke ambaye kwa sasa anashikiliwa katika hospitali ya Tawam licha ya kwamba anasumbuliwa na saratani ya titi.

Wataalam wa haki za binadamu watoa wito kwa mahakama  Misri kusitisha adhabu ya kifo

Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa hii leo mjini Geneva Uswisi wamelaani kitendo cha kuteswa na kuuawa kwa wanaume tisa nchini Misri.

Mwaka 2018 ulikuwa mbaya zaidi kwa watoto Afghanistani- Ripoti

Zaidi ya watu 3,800 waliuawa mwaka jana nchini Afghanistani kutokana na mashambulio idadi ambayo ni ongezeko kwa asilimia 11 ikiliniganishwa na mwaka uliotangulia wa 2017.

Ghasia zashamiri Venezuela, raia 4 waripotiwa kuuawa

Umoja wa Mataifa umeelezea masikitiko yake makubwa kufuatia ghasia zinazoendelea kwenye mpaka wa Venezuela na mataifa ya Brazil na Colombia na ndani ya Venezuela kwenyewe ambapo sasa zimeripotiwa kusababisha vifo na majeruhi miongoni mwa raia.

OHCHR yatiwa wasiwasi na taarifa za watu 15 kunyongwa Misri

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR ina wasiwasi kuhusu taarifa kutoka Misri isemayo watu 15 wamenyongwa mwezi huu wa Februari ambapo watu tisa maisha yao yalikatiliwa isiku ya Jumatano wiki hii huku wengine sita walikabiliwa na hukumu ya kifo mapema mwezi huu.

Ajira bora ni muhimu katika kufikia haki ya kijamii:ILO

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya haki ya kijamii hii leo, Mkurugenzi mkuu wa shirika la kazi duniani ILO, Guy Rider amesema ajira bora ni muhimu sana katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu  na haki ya kijamii ambapo bila hivyo amani ya kudumu inakuwa ni ndoto.