Haki za binadamu

Ninawasihi Israeli sitisheni kinachoendelea mashariki mwa Jerusalem – Antonio Guterres  

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameelezea "wasiwasi wake mkubwa juu ya vurugu zinazoendelea Jerusalem Mashariki, na vile vile uwezekano wa kufukuzwa kwa familia za Wapalestina kutoka kwenye makazi yao katika maeneo ya Sheikh Jarrah na Silwan. 

Kutoka Mashinani: Manusura wa mzozo Uganda asaidia jamii kusonga mbele 

Mwanaume mmoja nchini Uganda ambaye amejiepusha kutumbukia katika mzozo wa miongo kadhaa nchini humo, kwa kuepuka kutumikishwa vitani akiwa mtoto, amejitolea utu uzima wake kuleta uponyaji kwa jamii ambazo zimeathiriwa na mapigano kati ya serikali na kikundi cha waasi cha Lord’s Resistance Army, LRA. 

Vyombo huru vya habari ni msingi wa jamii za kidemokrasia:UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo amezihimiza serikali "kufanya kila kila lililo ndani ya uwezo wao kusaidia uhuru wa vyombo vya habari, ambao kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ameutaja kama ni msingi wa jamii za kidemokrasia". 

UNESCO Tanzania yapatia wanahabari vifaa vya kujikinga na COVID-19 

Nchini Tanzania Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limepatia wanahabari nchini humo vifaa vya kujikinga na virusi vya Corona, au COVID-19 pindipo wanafanya majukumu yao. 

UNESCO leo imekabidhi tuzo ya Guillermo Cano kwa Maria Ressa

Mwandishi wa habari wa uchunguzi wa Ufilipino leo ametunukiwa tuzo  ya heshima kwenye hafla iliyoandaliwa iliyoandaliwa na Serikali ya Namibia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO katika mji mkuu Windhoek, nchini Namibia ambako wataalamu wa vyombo vya habari wanataka hatua za dharura zichukuliwe dhidi ya vitisho na kudhoofishwa kwa uhuru wa habari kote ulimwenguni.

Watu wenye ulemavu Burundi waamua kuutekeleza wito wa UN kwa vitendo 

Nchini Burundi, Dany Kasembe, mwenye ulemavu wa mguu, ameamua kuwashirikisha wenzake katika kuutekeleza wito wa Umoja wa Mataifa kwa vitendo, wito ambao unataka uwepo wa dunia ambayo watu wote wana uwezo wa kupata fursa sawa na pia ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu katika jamii ikiwemo katika hatua za kukabiliana na kujikwamua na janga la corona au COVID-19. 

Maria Ressa wa Ufilipino kupokea tuzo ya UNESCO ya Guillermo 2021

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limemtaja mwandishi wa habari za uchunguzi na mkuu wa vyombo vya habari Maria Ressa wa Ufilipino kuwa ndio mtunukiwa wa tuzo yake ya uhuru wa vyombo vya habari kwa mwaka 2021. 

Ripoti kuhusu kutokuwepo ubaguzi wa rangi wa kitaasisi Uingereza ni upotoshaji: Wataalam 

Wataalam huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wamelaani vikali ripoti inayoungwa mkono na serikali ya Uingereza kuhusu ubaguzi wakisema kwamba inapotosha zaidi na kuharamisha ukweli wa kihistoria kuhusu ubaguzi na kwamba inaweza kuchochea zaidi ubaguzi na ubaguzi wa rangi.  

Tunatiwa wasiwasi mkubwa na ukiukwaji wa haki za binadamu Uganda:UN 

Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wameiomba serikali ya Uganda isitishe mara moja ukandamizaji mkubwa dhidi ya wapinzani wake wa kisiasa ambao ulianza kabla ya uchaguzi mkuu wa Januari ulioleta mzozo na unaendelea kuwakandamiza wafuasi wa upinzani. 

Mzozo nchini Myanmar unaelekea kuwa vita kamili aonya Bachelet  

Ukandamizaji dhidi ya waandamanaji unaoendelea nchini Myanmar unaweza kusababisha mzozo kuwa vita kamili sawa na Syria, ameonya leo Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, akiyataka Mataifa yenye ushawishi kuchukua hatua za haraka na zenye ufanisi kukomesha mauaji ya raia nchino humo.