Haki za binadamu

Kongamano la kukabiliana na kauli za chuki yafungua pazia Geneva

Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi imefanya kongamano kwa ajili ya kukabiliana na kauli za chuki ili kulinda vikundi vidogo vya kidini, wakimbizi na wahamiaji.

Yemen acheni kuadhibu watu kwa misingi ya imani zao- Wataalamu

Watalaam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametaka mamlaka zilizoko hivi sasa Yemen kutupilia mbali mara moja adhabu ya kifo aliyohukumiwa Hamid Kamali bin Haydara, kwasababu tu ya kuwa muumini wa dini ya Bahá’í.

Tunalaani vikali shambulizi dhidi ya Sinagogi la Wayahudi Califonia:UNAOC

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Muungano wa ustaarabu UNAOC imetoa taarifa ya kulaani shambulio lililofanyika jumamosi nchini Marekani dhidi ya Sinagogi la Wayahudi.

WFP inahitaji kuongezewa nguvu ili kupambana na Ebola.

Wakati Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC ikipambana na mlipuko wa pili mkubwa wa ugonjwa wa Ebola, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limetahadharisha hii leo mjini Goma kuwa rasilimali zinazohitajika kusaidia shughuli zake, haziendani na kasi ya ongezeko la hivi karibuni la maambukizi na uwepo wa hatari ya kusambaa kwa virusi hivyo ndani ya DRC na katika nchi za jirani.

Ubunifu wa teknolojia usisigine haki za binadamu- Bachelet

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amesema ubunifu wowote wa teknolojia za kisasa usilenge kuingilia au kudidimiza haki za binadamu.

Zaidi ya Watoto 40 wameuawa katika mashambulizi ya Sri Lanka:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, leo limesema limeshtushwa sana na kusikitishwa na ukatili wa hali ya juu ulioelekezwa kwa familia wakiwemo Watoto waliokuwa wamekusanyika makanisani na hotelini wakati wa siku ya Pasaka nchini Sri Lanka.

Tunachukua hatua lakini ukatili wa kingono bado umeota mizizi- Guterres

Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wakati sasa umewadia kuchukua hatua mpya ili kutokomeza ukatili wa kingono kwenye mizozo, wakati huu ambapo vimeshamiri kuanzia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Sudan Kusini hadi Myanmar.

Watu zaidi ya 200 wauawa katika milipuko Sri Lanka, Umoja wa Mataifa na viongozi duniani walaani.

Zaidi ya watu 200 wameuawa na mamia kujeruhiwa kufuatia mfululizo wa wa milipuko ndani ya makanisa na hoteli kadhaa nchini Sri Lanka wakati wakristo wakijumuika kwa ajili ya misa ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka hii leo.

 

Watoto 6000 waunganishwa na familia zao nchini Sudan Kusini.

Idadi ya watoto waliouganishwa na familia zao nchini Sudan Kusini baada ya kutenganishwa kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza mwezi Disemba mwaka 2013 sasa imefikia 6000.

Kampeni ya #Vaccineswork kutumika mtandaoni kuimarisha utoaji chanjo- UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF tarehe 24 mwezi huu wa Aprili linazindua kampeni kamambe ya chanjo ili kukabiliana na ongezeko la milipuko  ya magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa chanjo.