Haki za binadamu

Navi Pillay ataka kuzingatiwa zaidi kwa ustawi wa wazee

Mkuu wa kamishna ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu Navi Pillay amesisitiza

haja ya kuwepo kwa sheria madhubuti kwa ajili ya kulinda ustawi wa watu wazee

ambao amesema licha ya kuendelea kuongezeka lakini bado hawajatupiwa jicho.

Nchi nyingi za Asia-Pacific bado zina sheria kandamizi kwa watu wenye HIV

Nchi nyingi zilizoko katika eneo la Asia-Pacific zimetajwa kwamba bado

zimeendeleea kukumbatia sheria ambazo zinawanyima haki watu wanaoishi na virusi

vya HIV na wakati huo huo hazijatoa zingatio la kuwalinda wale ambao wapo

hatarini kuingia kwenye maambukizi hayo.

Pillay aitaka Bahrain kuheshimu uhuru wa watu kuandamana.

Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadamu Navi Pillay

ameelezea masikitiko yake kwa utawala wa Bahrain ambao amedai umekwenda mbali

mno kwa kutumia nguvu za dola ili kudhibiti maandamano ya wananchi ambao

wamechoshwa na mwenendo wa serikali yao

UNHCR yatilia shaka wakimbizi wanaoingia Italia

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR imesema hali mbaya ya

kisiasa inayoandama maeneo ya Kaskazini mwa afrika na mashariki ya kati inaweza

kuchangia pakubwa kuwepo kwa ongezeko la wahamiaji wanakimbilia nchi za ulaya

kupitia bahari ya Mediterranean.

Taasisi za kimataifa zimeshindwa kuwalinda waandishi wa habari:CPJ

Taasisi za kimataifa ambazo zinawajibika kulinda uhuru wa vyombo vya habari

zimelaumiwa kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake huku ulimwengu ukishuhudia

waandishi wa habari wakiendelea kukabiliwa na hali za vitisho, kuwekwa

magerezani na wengine kuuwawa.

Leo ni siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya watoto jeshini

Dunia leo inaadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga matumisi ya watoto jeshini, jambo ambalo ni uhalifu wa kivita.

Baada ya siku 18 hatimaye Rais Hosni Mubarak ajiuzulu Misri

Hatimaye baada ya siku 18 za maandamano ya mamilioni ya watu katika miji mikubwa nchini Misri Rais Hosni Mubaraka amejiuzulu.

Israel ni lazima isitishe ujenzi wa makazi ya walowezi:Pillay

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameitaka Israel isitishe ujenzi wa makaazi ya walowezi wa kiyahudi kwenye ardhi ya wapalestina.

Hatua za haraka zinahitajika kutatua mzozo wa Ivory Coast:UNHCR

Mvutano wa kisiasa nchini Ivory Coast hadi leo umewatawanya watu zaidi ya 70,000 limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Lazima tuungane kuhakikisha holocaust haitokei tena:BAN

MUSIC HOLOCAUST CEREMONY)

Hivyo ndivyo ilivyokuwa katika hafla maalumu ya kuwakumbunga wahanga wa mauaji ya Holocaust iliyofanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York ikiwa na kauli mbiu "Wanawake na Holocaust, ujasiri na upendo"