Haki za binadamu

Myanmar achia huru waandishi wa habari wa Reuters -UN

Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wana wasiwasi baada ya  mahakama nchini Myanmar kuwafungulia rasmi mashtaka waandishi wa habari wawili wa shirika la habari la Reuters.

Kenya hakikisha sekta ya biashara inazingatia haki za binadamu- Wataalam 

Kikundi kazi cha wataalam wa Umoja wa Mataifa juu ya biashara na haki za binadamu kimehimiza mamlaka nchini Kenya kutekeleza kwa vitendo mapendekezo yaliyotajwa katika Katiba ya nchi hiyo ya 2010 ya kuhakikisha biashara zinaheshimu haki za binadamu.

Tunapata changamoto tunaposaka kubadili sheria zinazokinzana na maadili ya kijadi- Liberia

Kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa  imehitimisha hii leo mapitio ya ripoti ya awali ya Liberia juu ya utekelezaji wake wa vipengele vya agano la kimataifa la haki za kiraia na kisiasa nchini.

Hukumu ya SPLA dhidi ya tukio la hoteli ya Terrain itangazwe:Patten

Pramila Patten, msaidizi wa Katibu Mkuu na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingono kwenye mizozo, leo ametoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini kutangaza hukumu ya kesi inayohusiana na tukio lililofanyika  kwenye hoteli ya Terrain .

Ukatili dhidi ya raia Sudan Kusini ni wa kutisha- ripoti

Wafuatiliaji wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamebaini ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanyika kwa makusudi dhidi ya raia ikiwemo ubakaji wanawake kwa magenge na watoto wenye umri mdogo hadi miaka minne. 

UN yashikamana na Msumbiji kuimarisha ulinzi wa wafanyakazi wahamiaji

Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la wahamiaji IOM, la kazi ILO na ofisi ya Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa yameshikama na serikali ya Msumbiji kuhakikisha ulinzi kwa wafanyakazi wahamiaji.

IOM yasaka dola milioni 2.1 kunusuru wasaka hifadhi walionasa Chad

Shirika la uhamiaij la Umoja wa Mataifa, IOM, linasaka zaidi ya dola milioni mbili ili kukidhi mahitaji ya dharura ya wahamiaji waliokwama na walio kwenye vituo vya mpito nchini Chad.
 

Utambuzi wa warohingya huko Bangladesh waendelea

Hatimaye warohingya wanapatiwa vitambulisho, ikiwa ni mara ya kwanza katika maisha yao. Vitambulisho hivyo ni vya ukimbizi huko Bangladesh.

Kuolewa ni changamoto kubwa kwa mwanamke mwenye ulemavu-Seneta Mwaura

Unyanyapaa bado upo kati ya wanawake na wanaume walio na ulemavu katika masuala mbalimbali kwenye jamii ikiwemo katika ufikiaji wa huduma muhimu na za msingi.  Hiyo ni kauli ya Seneta Isaac Mwaura kutoka Kenya katika mahojiano maalum na Idhaa ya Kiswahili.

Maelfu ya watoto wazidi kutoweka DRC

Maelfu ya watoto wametoweka kusikojulikana katika jimbo la Tanganyika nchini Jamuri ya kidemokrasia ya Congo DRC, na mama zao wamejotokeza na kupaza sauti wakitaka watoto wao warudishwe.