Haki za binadamu

India sheria yenu dhidi ya usafirishaji  haramu wa watu iende sanjari na haki za binadamu :UN

Serikali ya India imeshauriwa kudurusu  tena sheria yake mpya yenye nia ya kukabiliana na usfirishaji haramu wa binadamu  ili kuhakikisha hatua zinazopendekezwa zinakwenda sanjari na sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Licha ya hatua zinazochukuliwa ukatili wa kijinsia bado mtihani Tanzania

Ukatili wa kijinsia hususan kwa wanawake na watoto unaendelea kutoa changamoto kubwa nchini Tanzania.

Manusura wa kujilipua ageuka mtoa msaada wa sheria kwa wasichana

Msichana mmoja nchini Chad ambaye alinusurika kuuwa na bomu alililobebeshwa na Boko Haram ili kufanya mauaji, ameamua kuwa mtoaji wa msaada wa sheria kwa  kwenye ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA huko Bol nchini Chad. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Mateso dhidi ya warohingya huko Myanmar bado yaendelea- Wataalamu

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamehitimisha ziara yao ya siku tano nchini Bangladesh ambako walipata fursa ya kuzungumza na wakimbizi wapya wa kabila la Rohingya ambao wanamimnika nchini humo kutokana na mateso wanayopata nchini kwao Myanmar.

Tunapomuenzi Mandelea tuenzi kwa vitendo aliyoyakumbatia:UN

Nelson Mandelea alikuwa mtu wa vitendo na sio maneno matupu, tunapomuenzi tufanye hivyo kwa vitendo. Wito huo umetolewa hii leo kwenye na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwenye tukio maalumu la kumbukizi ya Mandela ambae angekuwa hai hii leo angekuwa na umri wa miaka 100 .

“Madiba” akumbukwa kwa uvumilivu wake- Guterres

Leo ni kumbukizi ya miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Rais wa kwanza mwafrika wa Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela.

Machafuko yenye mlengo wa kijamii Mopti Mali yatutia hofu:UN

Machafuko yenye mwelekeo wa kijamii yanayoendelea katika jimbo la Mopti katikati mwa nchi ya Mali yanatia wasiwasi mkubwa kwa mujibu wa ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa.

Wasichana wanastahili haki sawa na wavulana katika michezo: Maraam

Katika harakati za kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya watoto wa kike, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limeanzisha programu maalum ya mchezo wa mpira wa miguu au  kabumbu katika kambi ya wakimbizi ya Za’atari  nchini Jordan ili kutoa fursa kwa watoto hao wa kike na wasichana kufanya mazoezi.

Idadi ya raia waliouawa na kujeruhiwa Afghanistan 2018 imefurutu ada:UNAMA

Takwimu ziliotolewa leo na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA, zinaonyesha kuendelea kwa idadi ya mauaji na kujeruhiwa kwa raia kunakochangiwa na pande zote katika mzozo nchini Afghanistan.

Watu 800,000 wanakabiliwa na baridi kali na mvua kubwa Ethiopia-IOM

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, limesema, zaidi ya wakimbizi wa ndani 800,000 nchini Ethiopia wanaishi bila makazi ya kutosha na huduma ya kujisafi na hivyo kusababisha kuzorota kwa hali ya kibinadamu inayochochewa na  baridi kali na mvua.