Haki za binadamu

UN yalaani mauaji ya raia 200 yaliyofanywa na ISIL Syria

Umoja wa Mataifa  umelaani shambulio la kutisha lililofanywa na magaidi wa ISIL kwenye maeneo yanayokaliwa na raia wengi huko jimbo la As-Sweida kusini-magharibi mwa Syria.

Ugumu wa maisha ulichukua ujana wangu

Ugumu wa maisha unaowakabili wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo  DRC, ni moja ya vichocheo vya wazazi kulazimika kuwaoza watoto wao.

Kenya sitisheni kuwafurusha wakazi wa Kibera si haki:UN

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamelaani hatua ya serikali ya Kenya ya kuwafurusha wakazi wa mitaa ya mabanda ya Kibera mjini Nairobi na kuitaka serikali kusitisha mara moja zoezi hilo hadi pale hatua za kisheria zitakapokamilika.

Kasi ya maisha inawasahau wazee-Dkt.Wachira

Usemi usemao “ya kale ni dhahabu” waonekana kupitwa na wakati, sio tu katika familia ambazo kwa miaka nenda miaka rudi zimekuwa zikiamini wazee ndio dhahabu inayoshikilia jamii kwani kadri wanavyozeeka ndivyo wanaongeza maarifa watakayoavichia vizazi vya sasa na vijavyo hususan barani Afrika.

Licha ya hatua zinazochukuliwa ukatili wa kijinsia bado mtihani Tanzania

Ukatili wa kijinsia hususan kwa wanawake na watoto unaendelea kutoa changamoto kubwa nchini Tanzania.

Manusura wa kujilipua ageuka mtoa msaada wa sheria kwa wasichana

Msichana mmoja nchini Chad ambaye alinusurika kuuwa na bomu alililobebeshwa na Boko Haram ili kufanya mauaji, ameamua kuwa mtoaji wa msaada wa sheria kwa  kwenye ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA huko Bol nchini Chad. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

“Madiba” akumbukwa kwa uvumilivu wake- Guterres

Leo ni kumbukizi ya miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Rais wa kwanza mwafrika wa Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela.

Machafuko yenye mlengo wa kijamii Mopti Mali yatutia hofu:UN

Machafuko yenye mwelekeo wa kijamii yanayoendelea katika jimbo la Mopti katikati mwa nchi ya Mali yanatia wasiwasi mkubwa kwa mujibu wa ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa.

Wasichana wanastahili haki sawa na wavulana katika michezo: Maraam

Katika harakati za kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya watoto wa kike, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limeanzisha programu maalum ya mchezo wa mpira wa miguu au  kabumbu katika kambi ya wakimbizi ya Za’atari  nchini Jordan ili kutoa fursa kwa watoto hao wa kike na wasichana kufanya mazoezi.

Kenya hakikisha sekta ya biashara inazingatia haki za binadamu- Wataalam 

Kikundi kazi cha wataalam wa Umoja wa Mataifa juu ya biashara na haki za binadamu kimehimiza mamlaka nchini Kenya kutekeleza kwa vitendo mapendekezo yaliyotajwa katika Katiba ya nchi hiyo ya 2010 ya kuhakikisha biashara zinaheshimu haki za binadamu.