Haki za binadamu

Kamati kuhusu utesaji kurejea Rwanda-UN

Kamati ndogo ya Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia  utesaji-SPT-imeamua kurejea Rwanda baada ya kusimamisha uchugunzi huo, Oktoba 2017, ingawa tarehe  ya kurejea huko haijatangazwa.Kamati hiyo pia imesema itazuru Uruguay, Belize na Ureno.

Muongozo mpya kuhusu haki za waomba hifadhi watolewa: UN

Kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya utesaji (CAT) leo imetoa muongozo mpya kuhusu haki za waomba hifadhi.

Malengo ya SDGs hayotofanikiwa tusipotokomeza ubaguzi: Sidibe

Azima ya kuhakikisha afya kwa wote au malengo ya maendeleo endelevu SDGs havitoweza kufikiwa endapo dunia haitoukabili na kuutokomeza ubaguzi. 

Misaada ya kujikwamua ni muhimu zaidi kwa wakimbizi Chad

Naibu Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na  usaidizi wa majanga, OCHA, Ursula Mueller amehitimisha ziara yake huko Chad iliyolenga kujionea hali halisi ya athari za mashambulizi yanayofanywa na Boko Haram. 

Bila hatua za haraka tatizo la njaa Sudan kusini ni janga lisilo kwepeka: FAO

Ripoti ya shirika la chakula na kilimo duniani FAO iliyotolewa leo imebaini kuwa zaidi ya watu milioni 7 wako hatarini kukabiliwa  na janga  la njaa  ambalo halijawahi kutokea katika siku za usonii, nchini Sudan kusini. Hivyo msaada wahitajika haraka  ili kuokoa maisha ya wengi. Selina Jerobon na tarifa kamili

Je unawezaje kumudu saratani ukiwa ukimbizini bila fedha?

Hali ya kuwa mkimbizi ni mtihani tosha, ukiongeza changamoto za kiafya kama saratani , ambapo hata huduma za afya huwezi kumudu  inakuwaje? 

Guterres alaani mashambilizi ya kigaidi Moghadishu

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia msemaji wake amelaani mashambilizi ya kigaidi mjini Moghadishu yaliyotokea jana tarehe 23  na kukatili maisha raia wasio na hatia na kujeruhi wengine wengi

Mauritania yapatia vyeti vya kuzaliwa wakimbizi wa Mali

Heko Mauritania kwa kuanza kuwapatia vyeti vya kuzaliwa watoto ambao ni wakimbizi kutoka Mali walioko nchini  humo.

Wakimbizi wauawa na wengine kujeruhiwa Rwanda, UNHCR yashtushwa

Wakimbizi watano kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC wameuawa na wengine  wengi, mkiwemo afisa wa polisi kujeruhiwa, wakati vikosi vya usalama vilipokuwa vinajaribu kuzima maandamano ya wakimbizi wa kambi ya  Kiziba  magharibi mwa Rwanda. 

Uhamiaji ni suala mtambuka, wabunge walivalia njua: UN

Wabunge kutoka nchi mbalimbali duniani wanakutana makao makuu ya Umoja wa Mataifa  mjini New York Marekani kubadilisha mawazo ya jinsi ya kukabiliana na suala mtambuka la uhamiaji.