Haki za binadamu

Kamanda wa zamani wa LRA akutwa na hatia na ICC pasipo shaka yoyote

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, imempata na hatia za jumla ya makosa 61 Dominic Ongwen, kamanda wa zamani wa kundi la Lord’s Resistance Army, LRA la Uganda. 

Marekani kubadili mfumo wa kuomba hifadhi uhamiaji na kuunganisha familia. 

Shirika la Umoja la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limefarijika na hatua ya serikali ya Marekani, Jumannene kutia saini maagizo yanayolenga kutoa usalama na suluhu kwa wale wanaosaka hifadhi kwa misingi kwamba wanahitaji ulinzi kutokana na machafuko na mateso katika nchi zao. 

UN yasikitishwa na hukumu ya kifungo dhidi ya mpinzani wa kisiasa Urusi

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCR, imeelezea masikitiko  yake kufuatia hukumu ya kifungo dhidi ya mpinzani wa kisiasa na mwanaharakati nchini Urusi, Aleksei Navalny.
 

Tuna hofu na mwenendo wa kesi dhidi ya Dmitriev- Wataalamu UN

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa Urusi kuhakikisha kuwa kesi dhidi ya mtetezi wa masuala ya historia na haki za binadamu nchini humo Yuri Alexeevich Dmitriev inakuwa ya haki.

Waasi wa ADF na vikosi vya ulinzi vya DRC walishambulia raia 2020- Ripoti

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR, inasikitishwa na ongezeko kubwa la matukio ya mashambulizi ya raia kwenye maenoe ya Irumu na Mambasa jimboni Ituri halikadhalika eneo la Beni katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

UN yakaribisha hatua za kwanza kuelekea utimizaji wa haki Sudan Kusini

Kamisheni ya haki za binadamu nchini Sudan Kusini imekaribisha leo maamuzi ya serikali ya Sudan Kusini kuendelea na mchakato wa kuunda mahakama ya maridhiano na mbinu zingine za sheria kwa ajili ya kushughulikia ukiukaji wa haki za binadamu uliotekelezwa wakati wa mzozo. 

Chonde chonde Iran msimnyonge Javid Dehghan: OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR leo imeitaka serikali ya Iran kusitisha mara moja hatua ya kutaka kumnyonga raia wa nchi hiyo anayedaiwa kuteswa hadi kukiri  kwamba ni mwanachama wa kundi la jihadi.

Mwaka 2020 ulikuwa wa kifo na sasa 2021 ni wa matumaini, tushirikiane- Guterres

Mwaka 2020 ulikuwa ni mwaka wa majanga lakini 2021 ni mwaka wa fursa na matumaini! Ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyotoa leo kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  jijini New York, Marekani akielezea vipaumbele vyake 10 kwa mwaka 2021. 

Zaidi ya watu 100,000 wamefurushwa makwao Darfur na kuna ripoti za ukiukwaji wa haki za binadamu-UN

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeelezea wasiwasi wake kufuatia kuongezeka kwa machafuko katika eneo la Darfur nchini Sudan ambayo yamesababisha maelfu ya watu kukimbia makwao na kusaka hifadhi ikiwemo mpakani nchini Chad. 

OHCHR inasikitishwa na ukiukaji wa haki za binadamu Haiti

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR, imeelezea wasiwasi wake kuhusu kuendelea kwa ukosefu wa usalama, umaskini, ukosefu wa usawa na kuongezeka kwa uhasama wa kisiasa ambao huenda ukachochea ghadhabu kutoka kwa umma ambayo itafuatiwa na kukandamizwa na polisi na ukiukaji wa haki za binadamu.