Kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR tarehe 27 mwezi Desemba mwaka huu, wapiga kura kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui wametoa maoni yao wakati huu ambapo tayari kazi ya kuandikisha wapiga kura ilianza mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.