Viongozi wa jumuiya za ughaibuni na mashirika ya kijamii kutoka kote duniani wamekuja pamoja kutuma ujumbe ulio bayana na wa mshikamano na watu wanaokabiliwa na vitendo vya chuki dhidi ya wageni, ubaguzi na hata ukatili kutokana na janga la corona au COVID-19 kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.