Mila na desturi za kitamaduni zina mchango mkubwa katika jamii endapo zitaenziwa kwa kuheshimu haki zingine za binadamu. Hata hivyo wakati mwingine jamii hutumia haki za kitamaduni kama kisingizio cha kukandamiza wengine au kubinya haki zingine za binadamu katika jamii.
Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, #UDHR likitimiza miaka 70 mwezi disemba mwaka huu wa 2018, harakati mbalimbali zimekuwa zikifanyika ili kukumbusha binadamu haki zao za msingi zilizotajwa bayana ndani ya nyaraka hiyo yenye ibara 30.
Kesi ya mbabe wa zamani wa kivita kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Ntabo Ntaberi Cheka imeanza kusikilizwa mjini Goma jimbo la Kivu ya Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.
Nchini Sri Lanka, shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA na shirika moja liitwalo Cheer Up Luv wanafanya kampeni ya pamoja kukabiliana na unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake kwenye usafiri wa umma.
Ripoti mpya ya shirika la kazi duniani, ILO kuhusu kiwango cha mishara inaonyesha kuwa ongezeko la mishahara kote duniani kwa mwaka 2017 lilikuwa chini sana tangu mwaka 2008 na wanawake bado wanalipwa ujira mdogo kuliko wanaume.
Utafiti uliofanywa na shirika la kazi duniani, ILO huko Jordan, umebaini kuwepo kuwa wafanyakazi wa mashambani hususan wakimbizi kutoka Syria wanaoishi nchini humo wanafanya kazi katika mazingira magumu na hivyo hatua zinapaswa kuchukuliwa kuwaokoa.
Ibara ya 13 ya tamko la haki za binadamula Umoja wa Mataifa ambalo linatimiza miaka sabini mwaka huu inasema, kila mtu ana haki ya uhuru wa kutembea na kuishi ndani ya mipaka ya nchi yake - Na kila mtu ana haki ya kuondoka na kurudi nchini mwake.
Tanzania imepiga hatua katika utekelezaji wa baadhi ya haki za binadamu ikiwemo kuhakikisha haki za washitakiwa kudhaminiwa, au tutokuchukuliwa kuwa na hatia hadi itakapothibitishwa.
Ibara ya 9 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linalotimiza miaka 70 mwaka huu wa 2018, inaeleza kuwa hakuna mtu anayepaswa kukamatwa kiholela na kuwekwa ndani au kulazimishwa kwenda uhamishoni. Lakini je! Nchi wanachama zinatimiza matakwa ya ibara hii?