Wakati msafara wa mamia ya raia wa Amerika ya Kati ukiripotiwa kuvuka mpaka na kuingia Mexico mwishoni mwa wiki, mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za wahamiaji, Felipe Gonzalez, ametoa wito kwa nchi kutoziweka rehani haki za binadamu za wahamiaji hao kwa sababu ya hofu ya masuala ya usalama.