Tangu kupitishwa kwa mkataba wa haki za mtoto miaka 30 iliyopita pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana kote duniani bado vita imesalia kuwa chanzo kubwa ya ukiukwaji wa haki za mtoto na bado kuna nchi hazijaridhia mkataba huo amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Nchini Yemen, muhula mpya wa shule ukianza huku mzozo ukiendelea, watoto milioni 2 hawawezi kwenda shule, idadi ikijumuisha nusu milioni ambao ni watoro wa shule tangu mzozo uanze nchini humo mwaka 2015.
Leo ni siku ya kimataifa ya lugha za ishara ambayo kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni muhimu sana kuhakikisha takrikutomwacha yeyote nyuma.ban watu milioni 72 hawaachwi nyumba na treni ya kutimiza ajenda ya maendeleo ya 2030.
Hatimaye kikao cha kwanza cha mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kimeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani chini ya uongozi wa Rais wake Balozi Tijjani Muhammad-Bande kutoka Nigeria.
Mmoja wa wanawake waliobakwa mara kadhaa na magenge ya wahalifu huko Sudan Kusini amehoji ni hatua gani zitachukuliwa na kamisheni hiyo na jamii ya kimataifa ili kumnusuru yeye na wanaweke wengine waliokumbwa na madhila kama hayo huko Bentiu.
Serikali ya Rwanda, Shirika la Kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR na Muungano wa Afrika, AU leo hii wametia saini makubaliano ya kuanza mchakato wa kuhamisha wakimbizi kutoka Libya.
Mtoto mkimbizi kutoka Mynmar anayeishi Cox’s Bazar nchini Bangladesh amesema bila kujali mazingira anayoishi anataka kutimiza ndoto yake ya kusoma na kuwa mhandisi au daktari.
Ikiwa imesalia chini ya mwaka mmoja kuelekea kufanyika uchaguzi wa rais,wabunge na serikali za mitaa nchini Burundi mwakani 2020, kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuichunguza Burundi COIB imetoa ripoti yake hii leo mjini Geneva Uswisi na kusema kuwa kuwa kuna hali ya hofu na vitisho kwa watu wote ambao hawaonyeshi kukiunga mkono chama tawala cha CNDD-FDD. Grace Kaneiya na ripoti kamili.
Mwaka mmoja baada ya kushika jukumu la ukamishna wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet amesema hakutarajia kuwa itakuwa kazi rahisi, lakini amevunjwa moyo kutokana na mwelekeo wa haki za binadama hivi sasa. Assumpta Massoi na ripoti kamili.