Zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya wananchi wa Sudan Kusini kuanza kupiga kura ya maoni ya kuamua hatma yao hapo siku ya Jumapili ijayo, mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameutaka uongozi wa Sudan kuhakikisha kura ya maoni inakuwa huru na ya haki.