Haki za binadamu

Ghasia huenda zikazuka kufuatia kutajwa washukiwa wa machafuko Kenya:OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA ofisi ya Kenya limesema kutajwa kwa watu sita wanaoshukiwa kuchagiza machafuko ya baada ya uchaguzi Kenya kunaweza kuzusha ghasia katika baadhi ya jamii.

Baada ya ngojangoja Mwedesha Mashitaka wa ICC awataja vigogo sita waliohusika na machafuko Kenya

Mwendesha mashitaka mkuu wa Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC Luis Moreno Ocampo, amewataja vigogo sita nchini Kenya ambao wanashutumiwa kwa kuchochea ghasia zilizozuka baada ya uchaguzi mkuu wa Rais mwaka 2007.

Mafunzo dhidi ya usafirishaji haramu wa watu yafanywa Guinea Bissau

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM, limenza kuendesha mafunzo ya siku tatu kwa wataalamu mbalimbali nchini Guinea Bissau watakaotumika kuwasadia watu waliokubwa na matatizo ya usafirishaji haramu wa binadamu.

Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari kujikita katika habari na karne ya 21

Vyombo vya habari karne ya 21, mtazamo mpya na mipaka mipya hiyo ndio itakuwa kauli mbiu ya maadhimisho yajayo ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari hapo Mai 3 mwaka 2011.

Magenge ya usafirishaji haramu wa watu yadhibitiwe:Ban

Vitendo vya usafirishaji haramu wa binadamu vimeendelea kuwafadisha magenge machache ya watu huku wanawake na watoto wakiendelea kuwa wahanga wakubwa wa matukio hayo.

Wataalamu wa Haki za Binadamu wa UM wahofia kusumbuliwa kwa watetezi wa haki Uchina

Wataalamu watatu wa haki za binadamu wameelezea hofu yao dhidi ya kusumbuliwa na kukamatwa kwa watetezi wa haki za binadamu nchini Uchina tangu kutangazwa kupewa tuzo ya Nobel kwa mpigania haki Liu Xiaobo miezi miwili iliyopita.

Mwaka wa kimataifa wa watu wenye asili ya Kiafrika wazinduliwa

Mwaka wa kimataifa wa watu wenye asili ya Kiafrika umezinduliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani.

Vitisho kwa taarifa za mitandaoni havifai- Navi Pillay

Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu siyo jambo la haki kuendelea kuandamana mtandao mmoja ambao umechapisha ripoti za siri zinazohusu utendaji wa serikali ya Marekani.

Hatua za kuwazuia wahamiaji kuingia Ulaya kinawanyima nafasi wahamiaji halali:UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasema kuwa hatua zilizowekwa na Jumuiya ya Ulaya ili kudhibiti wahamiaji katika Bahari ya Mediterranean kunawanyima wahamiaji halali usalama wanaohitaji.

Mauaji ya halaiki yaendelea Darfur:ICC

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC amesema kuwa mauaji ya halaiki bado yanaendelea katika jimbo la Darfur nchini Sudan na kuwa Rais wa nchi hiyo Omar al-Bashir ambaye amepewa waranti wa kukamatwa na mahakama hiyo anaendelea kuficha na kuihadaa jamii ya kimataifa.