Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo akiwa mjini New York Marekani kabla ya kusafiri kwenda Argentina unakofanyika mkutano wa nchi 20 zilizoendelea zaidi kiuchumi G20, amewaambia wanahabari kuwa changamoto kubwa hivi sasa ni ukosefu wa kuaminiana duniani.
Nchini Sri Lanka, shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA na shirika moja liitwalo Cheer Up Luv wanafanya kampeni ya pamoja kukabiliana na unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake kwenye usafiri wa umma.
Katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja waandishi habari takriban elfu moja wameuawa wakati wanafanya kazi yao adhimu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kukomesha ukwepaji sheria kwa uhalifu dhidi ya waandishi wa habari.
Naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya nje wa Syria Walid al-Muallem amesema vita vya nchi yake dhidi ya ugaidi vinaelekea ukingoni akishukuru ujasiri, dhamira, umoja wa watu wa Syria, jeshi la nchi hiyo, msaada wa marafiki na washirika wao.
Umoja wa Mataifa na Muungano wa Ulaya EU leo wamezindua mkakati wa kukomesha mauaji dhidi ya wanawake na wasicha katika nchi tano za Amerika ya Kuisni kwa sababu tu ya jinsia yao, mkakati ujulikanao kama Spotlight.
Leo ni maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kumbukizi na kutoa heshima kwa wahanga wa ugaidi duniani, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ni fursa ya kusikiliza sauti zao pamoja na waathirika wa vitendo hivyo kama njia ya kufanikisha vita dhidi ya ugaidi duniani.
Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein amesema machungu wanayopitia wahanga wa ukiukwaji wa haki za binadamu ni shinikizo kubwa kwake yeye kuzungumza bila woga.
Wiki ya unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama ikianza hii leo, Umoja wa Mataifa umesema utashi wa kisiasa ndio muarobaini wa kufanikisha suala la kuwezesha mtoto kunyonya maziwa ya mama yake punde tu anapozaliwa.