Haki za binadamu

UM inayakumbusha makundi yanayohasimiana Kivu Kaskazini wajibu wa kisheria kulinda haki za raia

Navi Pillay, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu naye pia ameripoti wasiwasi kuhusu taarifa za kuzidi kwa mauaji ya kihorera na ukiukaji wa haki za binadamu uliosajiliwa kufanyika katika siku za karibuni katika jimbo la Kivu Kaskazini, kwenye JKK.

Kamati ya haki za walemavu kuteuliwa rasmi

Asubuhi ya leo, kwenye Makao Makuu ya UM mjini New York, kikao cha awali cha Mataifa Yalioridhia na Kuidhinisha Mkataba wa Haki za Watu Walemavu kilikutana rasmi kuchagua wajumbe 12 wa kutumikia Kamati juu ya Haki za Watu Walemavu. ~

M. Novak ahadharisha tabia karaha ya kufanya mateso kama desturi za kawaida

Mkariri/Mtaalamu Maalumu Huru wa UM juu ya Mateso, Manfred Novak Alkhamisi alihutubia Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la UM ambapo alihadharisha kwamba katika uchunguzi wake wa kimataifa amegundua na kuthibitisha ya kuwa vitendo vya mateso vinaendelea kufanywa desturi za kawaida katika nchi nyingi za dunia.

Kamishna wa Haki za Binadamu anasema umaskini unafungamana na utovu wa haki za kimsingi

Kamishana Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay, amekumbusha kwenye taarifa alioitoa kuhishimu Siku ya Kimataifa Kuangamiza Umaskini’ ya kwamba kuna fungamano halisi kati ya utekelezaji wa haki za binadamu na hali ya umaskini ulimwenguni.

Utekelezaji wa haki za binadamu utazingatiwa Nairobi kwenye mkutano wa kimataifa

Taasisi za Kimataifa kuhusu Haki za Binadamu kutokea nchi 71 zinatarajiwa kukusanyika mjini Nairobi, Kenya wiki ijayo kuzingataia masuala yanayohusu usimamizi wa haki kimataifa.

UM wakumbusha 'walio vizuizini wana haki za kiutu na lazima zihishimiwe'

Kamisheni ya UM juu ya Haki za Binadamu imeanzisha kampeni maalumu ya kimataifa itakayoendelezwa hadi Oktoba 12 (2008) ambapo taasisi za kizalendo zinazogombania haki za binadamu katika nchi wanachama wa UM, pamoja na mashirika yasio ya kiserikali na wadau wengine husika zitajumuika kukumbushana juu ya ulazima, na umuhimu, wa kuhakikisha watu waliowekwa vizuizini na kwenye magereza huwa wanatekelezewa haki zao zote halali za kimsingi.

Mkuu wa UNHCR atetea haki za mafakiri na wahamaji waliokosa makazi ulimwenguni

António Guterres Kamishna Mkuu wa Shirika la UM juu ya Wahamiaji (UNHCR) kwenye risala ya ufunguzi mbele ya wajumbe waliohudhuria mkutano wa mwaka Geneva wa Kamati ya Utendaji ya UNHCR, ya kwamba maslahi ya watu mafukara na wale waliong’olewa makwao ulimwenguni yamo hatarini sasa hivi, kwa sababu ya mchanganyiko wa athari mbalimbali zinazochochewa na migogoro iliofumka karibuni ya kiuchumi, kijamii na kisiasa, hali ambayo, alisema anakhofia itazusha watu kungo’lewa zaidi makazi katika miaka ijayo.