Takwimu ni muhimu sana ili kuonyesha ni kwa kiasi gani mwanamke wa kijijini anachangia katika uzalishaji na maendeleo hasa katika vita vya ukombozi wake.
Bila msaada wa kibinadamu maisha ya raia wengi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) yako mashakani. Onyo hilo limetolewa na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anaehusika na masuala ya kuratibu misaada ya kibinadamu , Mark Lowcock wakati akilihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hii leo na kuelezea hali ilivyo DRC.
Mpango wa pamoja wa kunusuru maelfu ya wakimbizi wa Rohingya kutokana na janga la kibinadamu, umezinduliwa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswis , ukihitaji dola zaidi ya milioni 900.
Wakati Umoja wa Mataifa na wadau wake wanapambana kukomesha ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake, serikali ya Tanzania nayo pia ipo mstari wa mbele kuhakikisha hakuna mwanamke au mtoto wa kike atakayebaki nyuma katika mpango huo madhubuti.
Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kibinadamu na kuratibu misaada ya dharura na waziri wa biashara ya nje na ushirikiano wa maendeleo wa Uholanzi, wamesema hali ya wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ni mbaya sana na hatua za haraka zahitajika kunusuru watu hao.
Umiliki wa ardhi hasa miongoni mwa wanawake bado unasalia kukumbwa na utata hasa kwenye nchi ambako mila na desturi potofu zimeshamiri ili kuzuia umiliki huo. Sasa wanaharakati wanapigia chepuo umiliki kamilifu ambao kwao mwanamke au msichana ataendelea kumiliki ardhi hata anapokuwa hajaolewa, ameolewa au amesalia mjane.
Mkutano wa 62 wa kamisheni ya hali ya wanawake, CSW62 uking'oa nanga hii leo, washiriki nao wanapaza sauti ni kipi wanafanya kubadili maisha ya wanawake wa vijijini. Leo tumezungumza na washiriki kutoka Monduli mkoani Arusha nchini Tanzania pamoja na kutoka kaunti ya Kwale huko Mombasa nchini Kenya.
Kamishna mkuu wa haki za binadamu, Zeid Ra’ad Al Hussein amekemea hatua za utawala wa Ufilipino za kumuweka katika orodha ya magaidi, uwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za watu asili, Victoria Tauli-Corpuz.