Tanzania itatumia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kutangaza msimamo wake na chombo hicho chenye wanachama 193. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.
Umoja wa Mataifa leo umepitisha azimio la kumuenzi Nelson Mandela kutokana na mchango wake katika kusongesha utu, amani na haki za binadamu siyo tu nchini mwake bali duniani kote kwa ujumla. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.
Mwanadiplomasia nguli ambaye amewahi kufanya kazi na hayati Mzee Nelson Mandela azungumzia upekee aliokuwa nao mwendazake huyo ambaye leo anaenziwa na UN
Leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanapitisha azimio la kumuenzi aliyekuwa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela.
Nuru inaangazia nchini Kenye ambako nchi hiyo inaelekea kuwa bingwa wa kikanda katika kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi samabmba na kuwapatia huduma za afya na elimu.
Mahakama kuu zaidi nchini Ukraine imetoa uamuzi unaosaidia mamia kwa maelfu ya wazee, wakimbizi wa ndani na wakaazi katika maeneo yasiodhibitiwa na serikali kupata pensheni zao ambazo wamekosa tangu 2014.
Huko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu, MINUSCA unaendesha mafunzo yenye lengo la kupunguza ghasia na kuleta maelewano baina ya jamii, CVR.
Kamishna Mkuu mpya wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amehutubia kwa mara ya kwanza kikao cha Baraza la Haki za Binadamu la umoja huo huko Geneva, Uswisi na kugusia mambo kadhaa ikiwemo ukiukwaji haki za binadamu dhidi ya warohingywa na huko Syria.
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema itatiwa hofu kubwa na vitendo vya ukandamizaji na ghasia dhidi ya maandamano ya amani yanayofanywa na mashirika ya kiraia na upande wa upinzani wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.
Yumkini hali ya mambo bado si shwari kwenye mji mkuu wa Libya, Tripoli ambako tangu kuzuka machafuko wiki iliyopita takriban raia 21 wameuawa wakiwemo wanawake na watoto huku 16 wakijeruhiwa. Sasa Umoja wa Mataifa watoa wito kwa pande kinzani kuwanusuru raia hao.