Mahakakama ya uhalifu wa kivita nchini Cambodia ambayo inaungwa mkono na Umoja wa Mataifa imekamilisha kusikiliza rufani ya watuhumiwa wa uhalifu uliofanywa wakati wa kiongozi wa zamani wa taifa hilo Khmer Rouge.
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kidini au imani Heiner Bielefeldt amepongeza mazingira ya uwazi na kuvumiliana nchini Paraguay katika ngazi ya jamii na serikali kwa ujumla.
Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu madeni ya nje na haki za binadamu Cephas Lumina amepongeza mfumo wa maendeleo wa Vietnam ambao unamuweka raia wa nchi hiyo kuwa kitovu cha maendeleo ya taifa.
Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa Mohamed Chande Othman amesema hali ilivyo katika jimbo la Abyei ni ya kuvunja moyo kutokana na kuendelea kujiri kwa matukio ya uvunjifu wa amani ambayo yanaweza kuvuruga juhudi za kuleta amani kwa Sudan nzima.