Leo ni siku ya watu wenye ulemavu ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa ujumbe wake akisema kuwa, “tunapolinda haki za watu wenye ulemavu, tunasonga mbele kufikia ahadi kuu ya Ajenda ya 2030 - kutowaacha yeyote nyuma,” akisema kuwa, hata hivyo bado kuna mengi ya kufanya, tumeona maendeleo muhimu katika kujenga ulimwengu jumuishi kwa wote.