Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki ya utamaduni Farida Shaheed ameishauri serikali ya Austria kuutambua utamuduni na kuuinua kwa kuuunga mkono.
Kamati ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na haki za wahamiaji wameelezea hofu kubwa waliyonayo kuhusu kunyanyaswa kwa wafanyakazi wahamiaji na familia zao nchini Libya na hasa wahamiaji kutoka nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara.
Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameeelezea kushangazwa kwake kufuatia kuendelea kuripotiwa visa vya mauaji ya waandamanaji na vikosi vya usalama nchini Syria.
Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limewateua wataalamu watatu ambao watachunguza madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Ivory Coast kufuatia ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa urais uliokumbwa na utata.
Mtaalamu wa kujitegemea anayefanya kazi na umoja wa mataifa katika masuala ya mateso Juan Mendez amesema kuwa amesikitishwa na kuvunjwa moyo baada ya kushindwa kuonana na askari mmoja anashikiliwa na serikali ya Marekani.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo amesisitiza haja ya haraka ya kuimarisha utawala wa sheria duniani,akisema unaweza kusaidia kukabiliana na baadhi ya changamoto zinazoikabili jumuiya ya kimataifa hivi sasa.
Serikali ya Kenya imelitaka baraza la usalama kujadili barua yake ya hoja ya kutaka kesi dhidi ya raia wake inayoendehswa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC ihairishwe.
Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na kutetea haki ya kutoa maoni na kusema Frank La Rue anatarajiwa kufanya ziara yake ya kwanza nchini Algeria kati ya tarehe 10 na 17 mwezi huu kufuatia mwaliko wa serikali.
Kundi la Umoja wa Mataifa linalohusika na kuchunguza matumizi ya mamluki na kufuatia visa vilivyoshuhudiwa nchini Ivory Coast na Libya limeonya kuwa bado mamluki wanatumika barani afrika ambapo wanalipwa kuwashambulia raia.
Makundi ya kutetea haki za binadamau yanayochunguza madai ya mauji na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu magharibi mwa Ivory Coast yamepata miili 100 zaidi kwenye miji tofauti kwa muda wa masaa 24 yaliyopita.