Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa Mohamed Chande Othman amesema hali ilivyo katika jimbo la Abyei ni ya kuvunja moyo kutokana na kuendelea kujiri kwa matukio ya uvunjifu wa amani ambayo yanaweza kuvuruga juhudi za kuleta amani kwa Sudan nzima.
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM kwa kushirikiana na serikali ya China leo wanatazamiwa kuendesha mafunzo ya siku tatu ambayo yanalenga kuwasaidia watu waliokumbwa na vitendo vya usafirishaji haramu wa binadamu
Mtaalamu wa kujitegemea wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadmu Michel Forts, amewataka wagombea urais nchini Haiti kutilia msukumu kuondosha mfumo wa kukwepa kuwajibisha pindi wapokwenda kinyume na haki za binadamu.
Serikali ya Uchina imetakiwa na mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la sayansi, elimu na utamaduni UNESCO kuchunguza kifo cha mwandishi habari wa Kichina Sun Hongjie.