Kesi ya viongozi wawili wa Kihutu kutoka Rwanda wanaoshutumiwa kuandaa mauji Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeanza mjini Stuttgart Ujerumani.
Mashirika yakiwemo shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF na lile la Save the Children yanasema kuwa biashara inastahili kuchangia katika kuweka viwango vya kibiashara vya kimataifa kuambatana na haki za watoto.
Leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari na kauli mbiu mwaka huu ni "vyombo vya habari karne ya 21, mipaka mipya na vikwazo vipya" ikijikita katika ongezeko la jukumu la internet na mtandao mpya wa mawasiliano.
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika kuchagiza na kulinda haki ya uhuru wa maoni na kujieleza Frank La Rue amesema serikali lazima zichangie na kuleta mabadiliko badala ya kukandamiza watu.
Watu takribani wanane wameuawa nchini Uganda na wengine wengi kujeruhiwa wakati majeshi ya usalama yalipowakabili waandamanaji waliokuwa wakipinga kupanda kwa gharama za maisha.
Kifo cha kiongozi wa Al Qaeida Osama Bin Laden pia kimetoa afueni kwa maelfu ya watu kwenye nchi za Afrika ya Mashariki hususani Kenya na Tanzania ambako mamia ya watu waliuawa katika shambulio la kwanza la kigaidi eneo hilo mwaka 1998.
Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limewaokoa watoto 20 waliokuwa wakisafirishwa kinyume cha sheria kwenye ziwa Volta nchini Ghana uokoaji unaojiri wakati ufadhili wa mradi huo unapofikia kikomo mwaka huu.
Mkuu wa shirika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Navi Pillay amekamilisha ziara ya siku mbili nchini Mauritania ambapo alizungumzia changamoto za masuala ya haki binadamu zinazoikabili nchi hiyo na maafisa wa ngazi za juu serikalini pamoja na waakilishi wa mashirika ya umma.